Chama cha Wananchi, CUF, Zanzibar, kimeelezea kushtushwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Kiengereza usiku wa Agosti 7 katika maeneo ya Mji Mkongwe Zanzibar
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Salim Biman,
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma
ilisema CUF inalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili la kuwamwagia
tindi wageni hao ,na kinawataka polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wa
kina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na
tukio hilo la kikatili wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
Taarifa hiyo ilisema: “Matokeo haya ya kikatili ya
kumwagiwa kwa watu tindikali yamekuwa yakishamiri siku hadi siku ndani
ya Visiwa vya Zanzibar,ambayo yamekuwa yamewathiri watu kadhaa tena bila
ya wahusika kupatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria kiasi ambacho
sasa jamii ya Wazanzibar imejengeka katika hofu juu ya usalama wa maisha
yao ya kila siku.”
Ilisema taarifa hiyo: “Hii ni dalili mbaya kwa
Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni
masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi wa Visiwa vyetu.
CUF ilisema tukio hilo kwa wageni hao waliokuwa
wakifanya kazi ya kufundisha shule za msingi kwa kujitolea ni la
kusikitisha na linahujumu elimu na sekta ya utalii Zanzibar na kwamba
wakati umefika kwa kila Mzanzibari kupinga.
kwa dhatimb.
iokuwa wakijitolea Zanzibar kwa kazi za usomesha
katika skuli za msingi hiri kuwa Sekta muhimu inayotegemewa katika
kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.”
CUF inawataka wananchi wote wa Zanzibar kutoa kila
aina ya ushirikiano kuweza kufanikisha kukamatwa wahalifu hao na
hatimaye kufikishwa katika sehemu husika.
‘‘Sambamba na hilo Chama cha Wananchi kinawataka
wananchi wote, polisi jamii kutoa kila aina ya ushirikiano kwa polisi
ili waweze kukomesha kabisa vitendo vyote vya kihalifu ndani ya nchi kwa
lengo la kuiendeleza sifa ya asili ya Zanzibar isemayo kuwa Zanzibar ni
njema atakae na aje’’ ilisema taarifa hiyo
No comments: