Hisia kali zimezuka nchini Uganda kufuatia hatua ya Bunge la nchi kupitisha mswada unaonuia kuharamisha maandamano ya umma
Wakosoaji wanasema kuwa huu ni ukandamizaji wa haki na uhuru wa watu kukongamana
Watetezi wa mswada huu wanasema unanuia kuleta uthabiti, huku wakosoaji wakisema ni njama ya serikali kuzima upinzani.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa mswada huo ni hatari sana kwa uhuru wa watu kuandamana nchini humo.
Mswada huo ulipitishwa licha ya kukosolewa sana
na makundi ya kidini , wabunge wa upinzani na umma kwa ujumla pamoja na
mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Kuanzia sasa polisi watahitajika kutoa idhini
kwa hata watu watatu wanaokusanyika katika sehemu za umma kujadili
maswala ya kisiasa.
Wanaouunga mkono mswaada huo wanasisitiza kuwa hauna nia mbaya ndani yake bali unaweza kutekelezwa.
Shirika la Amnesty linasema kuwa mswada huo ni
sehemu ya ukandamizaji na hata ishara yake ikiwa kufungwa magazeti
mawili na vituo viwili ya redio mnamo mwezi Mei mwaka huu kwa kuripoti
madai ya njama ya serikali kutaka kuwaua wanasiasa wa upinzani.
Mswada huo ulipendekezwa mwaka 2009 na hatimaye kupitishwa kufuatia miezi kadhaa ya mijadala mikali nje na ndani ya bunge.
Ilipitishwa na bunge ambalo wabunge wengi wa chama cha rais Yoweri Museveni (NRM), licha ya upinzani mkali ndani ya bunge.
Mswada huo unawapa polisi nguvu za kuhoji
mikutano yoyote ya hata watu watatu katika maeneo ya umma ya watu
wanaojadili mambo ya kisiasa.
Polisi pia watakuwa na uwezo wa kuvunja mikutano ya zaidi ya watu watatu wanajadili maswala ya kisiasa majumbani kwao.
Polisi lazima wapokee maombi ya watu wanaotaka
kukutana siku saba kabla ya kuwapa idhini na mikutnao inaweza tu
kufanyika kati ya saa sita mchana na saa sita jioni
No comments: