Ads Top

MOTO WAZUKA UWANJA WA NDEGE JOMO KINYATTA

 Huduma za usafiri wa ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya zimesimamishwa kwa muda na hakuna anayeruhusiwa kuingia katika uwanja huo kufuatia moto ilioliopuka majira ya asubuhi ya leo katika moja ya majengo katika uwanja huo
Kwa mujibu wa mkuu wa vipindi wa K 24 David Mbatia amesema chanzo cha moto huo unaoendelea kudhibitiwa na vikosi vwa zimamoto bado hakijafahamika japo kuwa hata hapo jana kumekuwa na kuchelewesha kuondoka kwa ndege kadhaa
Aidha mpaka sasa hakuna madhara kwa binadamu yaliyoripotiwa na kwamba jengo linalodaiwa kuathiriwa ni katika eneo linalotumiwa na abiria kusubiria muda na ndege zao.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.