Ads Top

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameteua baraza jipya la mawaziri, baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake wiki jana


Sudan Kusini ilipata kujitawala kutoka kwa Sudan mwaka 2011

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali , baraza hilo litakuwa ndogo ikilinganishwa na hapo awali.
Angali anatarajiwa kutangaza makamu mpya wa rais baada ya pia kumfuta kazi aliyekuwa makamu wake Riek Machar.
Hatua ya rais kufuta baraza la mawaziri ilikuja kufuatia malumbano kuhusu mamlaka kati ya Rais Kiir na Machar.
Sudan iliyo na utajiri mkubwa wa mafuta, ilijipatia uhuru mwaka 2011, na kuifanya nchi hiyo kuwa taifa changa zaidi duniani.
Makundi mengi yaliyojihami yangali yanaendesha harakati zao nchini humo.
Marekani ilielezea wasiwasi kwa kufutwa kwa mawaziri ikisema kuwa huenda ikatikisa tena nchi hiyo.
Duru kutoka ofisi ya Kiir zilisema kuwa alichukua hatua hiyo ili kuimarisha utawala bora.
Mwandishi wa BBC nchini humo, Nyambura Wambugu anasema kuwa Bwana Kiir anataka kuona hisia za watu kuhusu uteuzi wake, kabla ya kumtangaza makamu wake wa rais.
Kiir alimteua gavana wa jimbo la Jonglei linalokumbwa na vurugu, kama waziri wake wa ulinzi.
Alikuwa kamanda mkuu wa wapiganaji wakati wa vita vya wenyewe kwa wenywe dhidi ya utawala wa Khartoum.
Zaidi ya watu 100,000 wametoroka makwao eneo la Jonglei katika miezi ya hivi karibuni.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.