SAKATA LA TOZO ZA LAIN ZA SIMU KWA KIASI CHA SHILINGI ELFU MOJA KWA KILA MWEZI LAJA KWA SURA MPYA

‘Vitu vingine ni too cheap (rahisi sana) , hii kodi ni sheria, jaribuni
kufikiria kuwa fedha hii kwa mwezi ni kwa ajili ya kupata maji,
barabara na mawasi liano’. Makinda
Wakati sakata la kodi ya simu ya Sh1,000 kwa kila laini ya simu kwa
mwezi, inayotakiwa kulipwa na watumiaji wa simu likiwa limerejeshwa
bungeni na Serikali, Spika wa Bunge, Anne Makinda ameibuka na kusema
fedha hiyo ni ndogo na kila Mtanzania ataweza kuilipa
Spika Makinda alishangazwa na Mtanzania anayeshindwa kupata
Sh1,000 kwa mwezi, kufafanua kuwa kama wananchi wataifanya nchi yao kuwa
rahisi, watalalamika na umaskini mpaka siku watakayokufa. Julai 30
mwaka huu, Waziri wa Fedha, William Mgimwa alikaririwa akisema suala
hilo litamalizwa bungeni kisheria na kwamba wameanza kutekeleza agizo la
Rais Jakaya Kikwete la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau
wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala na
kodi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali Kuu
(PAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Bajeti, Spika Makinda
alisema, “Haya maendeleo tunayoyataka sisi kama Watanzania yatapatikana
kwa kulipa kodi, hata vitabu vitakatifu vinasema kila mtu lazima
achangie,”alisema.
Alisema bila kukusanya kodi nchi itashindwa
kujiendesha na kusisitiza kuwa kama angeulizwa kuhusu masuala ya
ulipaji kodi angesema uanzishwe hata mfuko maalumu wa kuwasaidia vijana.
Alisema kwa kuwa suala hilo la kodi hivi sasa ni
sheria, mabadiliko yake ni lazima yarudi bungeni na kwamba haamini
katika kushindwa kulipa fedha hiyo. “Tunataka kufanya vitu vingi na hatuwezi
kuitegemea Serikali katika kila kitu sasa yenyewe itatoa wapi fedha.
Hayo ni maoni yangu lakini hiyo ni sheria,” alisisitiza Spika Makinda
No comments: