WATANZANIA KUWENI MAKINI KWANI VIBAKA WAGEUKA TISHIO KARIA KOO KUELEKEA MAANDALIZI YA SIKU KUU

Binti aliyevamiwa na viabaka

Kibaka akiwa chini ya ulinzi

Maskini binti kapata kovu bila sababu ya msingi, enyi vibaka, siku zenu zinakaribia.
Harakati
za kujiandaa na sikukuu ya Eid. Kama unavyojua watu kariakoo huongezeka
zaidi na vibaka nao hutumia mwanya huo kwaubize wa watu kutafuta
mahitaji yao.
Binti mmoja aliyekuwa katika pilikapilika za maandalizi ya sikukuu ya
Eid Kariakoo alikutwa na mkasa baada ya kibaka mmoja kutaka kumpora begi
lake la mkononi.
Binti
huyo hakuwa tayari kuachia begi lake kirahisi, kitendo ambaacho
kilimuudhi kibaka huyo na kumpelekea kumkata na kisu kiganjani binti
huyo na kumtishia asipige kelele kwa kuwa atamfanyia kitu mbaya.
Kwa ujasiri aliokuwa kuwa nao binti huyo alipiga kelele zilizopelekea
wasamaria wema katika eneo hilo kumsaidia na kumtia nguvuni kibaka huyo
eneo la Kariakoo kituo cha mabasi yaendayo Mbagala.
No comments: