Wataalamu wa kuchunguza mauaji kutoka nchini Marekani na Uingereza wamejiunga na kikosi cha wataalamu nchini Kenya kudadisi hali katika jengo la Westgate


Katibu wa baraza la mawaziri, Francis Kimemia amesema kuwa wataalamu
wa Kimataifa watasaidiana na wale wa Kenya kuchunguza jumba hilo na
kusisitiza kuwa Kenya itaongoza shughuli hiyo.
Kupitia kwa urusa wake wa Twitter, Kimemia
amesema kuwa maafisa wataendesha shughuli ya kuondoa vifusi ili kuodoa
mmili iliyonaswa katika jengo hilo.
Jengo la Westgate lilitekwa na magaidi Jumamosi mchana huku wakiwaua watu kiholela na kuwateka baadhi.
Takriban watu 61 waliuawa na magaidi hao wakiwemo maafisa sita wa usalama huku washukiwa wengine 11 wakikamatwa.
Bwana Kimemia amesema kuwa Rais Uhuru Kenyatta ameitisha mkutano maalum wa mawaziri hii leo kuhusu shambulizi hilo
Habari na BBCswahili.com
Habari na BBCswahili.com
No comments: