Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Apata Mapokezi ya Makubwa Kwenye Ufunguzi wa Mchezo wa Mpira Maarufu Kama American Football Nchini Marekani

Msafara wa Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbrod Slaa ukiwasili uwanjani

Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani akisalimiana na Dr Slaa

Mshindi wa Nobel Peace Price na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno

wakiwa
katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye
hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo,Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa
alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani

Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye

Viongozi
Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa ndiye mgeni
Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri

Uwanja ukiwa umefurika wapenzi wa mpira takribani laki moja.Picha na Chadema
Ni
mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi makubwa ambayo
Dr. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu kama
American football. Dr. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo kikuu
cha Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na
Georgia State. Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi
mbali mbali wa kitaifa na wa jimbo la Alabama
Akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “
Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo. Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.
Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu. Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football.
Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania. Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo.
Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa. Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha.
Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa

No comments: