MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI -CHADEMA ZITTO KABWE:' SOMA TAARIFA YA KUWASILISHA MUSWADA BINAFSI WA SHERIA KUFUTA SHERIA YA MAGAZETI
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe
Nimetoa
taarifa rasmi kwa katibu wa Bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge kwamba
katika mkutano ujao wa Bunge nitawasilisha muswada binafsi wa sheria
kufanya marekebisho ya sheria ya magazeti kwa lengo la kuifuta kabisa
sheria hiyo.
Madhumuni ya muswada huo ni;
Madhumuni ya muswada huo ni;
“kufuta
sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kwa sababu inakinzana na Katiba ya
Nchi kuhusu haki za Raia kupata habari na kwamba iliorodheshwa na tume
ya Nyalali ni sheria kandamizi’
Muswada
wenyewe nitauwalisilisha siku ya ijumaa ili uchapwe kwenye gazeti la
Serikali uweze kuingia kwenye shughuli za Bunge zitakazoanza tarehe 15
Oktoba 2013 kwa ngazi ya kamati.
No comments: