Michuano ya ligi ya Uropa ilienndelea hapo jana, katika kundi K Tottenham ya uingereza iliivutia chini Anzhi Makhachkala ya urusi huko Moscow kwa mabao mawili kwa bila
Tottenham yapachika bao
Katika Mechi nyingine Swansea ya uingereza iliishinda St Gallen ya uswizi kwa bao moja kwa bila na kuchukua uongozi katika kundi A
Wakati huo huo kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson
amesema kuwa ije jua ama mvua, kipa wake nambari moja ni Joe Hart.
Mlinda lango huyo wa Man City alilaumiwa na wakosoaji wengi katika mechi
ya Jumatano dhidi ya Bayern Munich wakisema kuwa uzembe wake uliingia
katika ngazi ya juu siku hiyo, na kuicha timu hiyo taabani mikononi mwa
Beyern iliyoicharaza mabao matatu kwa moja katika michuano ya klabu
bingwa ulaya.
Wakati Mashabiki wa Man City wakiuma vidole vyao
kuhusu utendakazi wa kipa wao, wapo baadhi ya Mashabiki wa Man U nao
wanaosema kocha David Moyes ameshindwa kazi lakini wamekumbushwa na
mtangulizi wake Sir Alex Fergeson kuwa Moyes anatosha. Ikiwa hilo ni
kweli au la itajulikana, viwanjani ila kwa sasa Man U inashikilia nafasi
ya kumi na mbili katika msimamo wa ligii ya Uingereza jambo ambao
limewaacha wengi kujiuliza hatima ya Man U wanaotetea taji hilo.
Na katika riadha mshindi wa mara mbili wa mbio
za mita mia mbili Mjamaica Veronica Campbell-Brown sasa yuko salama
lakini ameonywa na usimamizi wa ridha nchini humo dhidi ya kutumia dawa
zilizopigwa marufuku. Campbell-Brown ambaye awali alipigwa marufuku Juni
baada ya kukataa kuchunguzwa katika kikao kimoja cha riadha Mei,
alikabiliwa na jopo la watu watatu lililobuniwa kumchunguza na
kumwadhibu.
No comments: