TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA:WILAYA YA MBEYA MJINI- WATUHUMIWA 46 KATI YA WATUHUMIWA 105 WALIOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KUTOKANA KWA TUHUMA YA KUFANYA VURUGU NA UHARIBIFU WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya-Diwani Athuman(ACP)

MNAMO TAREHE 03.10.2013
WATUHUMIWA 46 KATI YA WATUHUMIWA 105 WALIOKAMATWA MAENEO YA
MWANJELWA,SOWETO,MAMA JOHN NA ILOMBA KWA TUHUMA ZA KUFANYA VURUGU
WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KUJIBU MASHTAKA YANAYOWAKABILI YA KUFANYA
FUJO/VURUGU NA UHARIBIFU WA MALI- BARABARA.
- AWALI MNAMO TAREHE 02.10.2013 MAJIRA KATI YA SAA 09:00HRS HADI SAA 17:47HRSHUKO KATIKA MAENEO YA MWANJELWA,SOWETO,MAMA JOHN NA ILOMBAKUNDI LA VIJANA WAKOROFI NA WASIO TAYARI KUTII SHERIA WALISHINIKIZA WAFANYABIASHA KUFUNGA BIASHARA ZAO NA KISHA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA NA BARABARA ZA MITAA KWA KUWEKA MAWE MAKUBWA, MAGOGO, KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KURUSHA OVYO MAWE KWA ASKARI POLISI HALI ILIYOSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA NA WANANCHI WA JIJI LA MBEYA KWA UJUMLA.
- KUFUATIA VURUGU HIZO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA WANANCHI LILIKABILIANA NAZO NA KUFANIKIWA KUREJESHA HALI YA AMANI.
- CHANZO CHA TUKIO HILIILIKUWA NI WAHALIFU/WAFANYAFUJO KUTUMIA KIVULI CHA MALALAMIKO/MANUNG’UNIKO YA WAFANYABIASHARA KWENYE ENEO LA KODI HUSUSANI CHANGAMOTO KWA WAFANYABIASHARAWADOGOWADOGO KUWA BEI YA MASHINE YA KI-ELEKRONIKI NI GHALI KIASI CHA TSH 800,000/= HIVYO WAO KUSHINDWA KUNUNUA.
- HATA HIVYO KABLA YA VURUGU HIZO TAREHE 01.10.2013 WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 300 WALIPATA FURSA YA KUKUTANA NA MKUU WA MKOA MHE ABBAS KANDORO WAKATI WAFANYABIASHARA HAO WALIPOKUWA NA SEMINA ILIYOANDALIWA NA MAOFISA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MBEYA.KATIKA KIKAO HICHO WALIMUELEZA MKUU WA MKOA MANUNG’UNIKO WALIYOKUWA NAYO IKIWA NIPAMOJA NA BEI YA MASHINE YA ELEKRONIKI INAYOFANYA KAZI YA KUTOA RISITIKWA WATEJA NA KUWEKA KUMBUKUMBU.
- JUMLA YA WATUHUMIWA 105 WALIKAMATWA NA JESHILA POLISIMKOA WA MBEYA MIONGONI MWAO WANAUME 103 NA WANAWAKE 2 KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI. AIDHA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA KWA WATUHUMIWA WENGINE 59WALIOKAMATWA KATIKA TUKIO HILO IKIWA NI PAMOJA NA KUPEWA DHAMANA WAKATI UCHUNGUZI DHIDI YAO UKIENDELEA.
- HAKUNA MADHARA MAKUBWA KWA BINADAMU AU MALIYALIYOTOKEA ISIPOKUWA UHARIBIFU WA KUCHOMA BARABARA
- KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI NA WAKAZI WA MBEYA KUTOICHEZEA AMANI ILIYOPO KWANI GHARAMA YA KUIRUDISHA NI KUBWA. AIDHA ANATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA KUENDELEA KUTAFUTA UFUMBUZI WA MATATIZO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO KWA KUJENGA HOJA KWA MISINGI YA KUTIISHERIA ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANAENDELEA KUTOA RAI YA KUENDELEA KUWAFICHUA WAHALIFU WAKIWEMO WAFANYA FUJO, VURUGU NA KUKATAA KUWAUNGA MKONO KATIKA MAOVU.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 02.10.2013
MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA HATWELO BARABARA YA
MBEYA/TUKUYU WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA LILIACHA NJIA NA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 37-40
NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO.
CHANZO NI MWENDO KASI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU
YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Signed by.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments: