Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia wameshambulia Ikulu ya Rais katika mji mkuu Mogadishu
Umoja wa mataifa unasema umefahamishwa kuwa rais wa nchi hiyo
hakujeruhiwa na yu salama na kwamba shambulizi la wanamgambo hao
lilitibuka.
Waziri wa mambo ya usalama wa nchi hiyo Abdi Karim Hussein, amesema baadhi ya washambuliaji wamefariki na wengine kukamatwa.
Kundi la Al- Shaabab linalopigana na utawala
nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema makabiliano
yangali yanaendelea.
Walianza mashambulizi yao, kwa kutumia gari
lililokuwa na bomu ndani yake kwa kuliegesha kando ya ukuta na kisha
kuanza kupigana ili kuweza kuingia ndani.
Milipuko mikubwa ilisikika pamoja na milio ya risasi.
Majeshi ya muungano wa Afrika yamekuwa
yakipambana na wapiganaji hao na hata kuwafurusha kutoka mji mkuu
Mogadishu. Hata hivyo bado wanadhibiti sehemu nyingi nje ya Mogadishu
No comments: