Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Tabora
mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya mabasi ya zamani
ambapo aliwaambia wananchi hao lazima watendaji wa serikali wawajibike
na kama hawawezi basi wawajibishwe ili uwajibikaji uwe tija kwa kuleta
maendeleo ya nchi .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tabora mjini
na kuwaambia kuwa CCM itaendelea kuwepo Madarakani kwani ndio chama
pekee kinachozungumzia maendeleo ya Tanzania na kuwajali wananchi wake.
Mbunge
wa Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na
Uratibu)akihutubia wakazi wa Tabora kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana na kumpa pongezi kwa kazi nzuri anayofanya ya
kujenga na kuimarisha chama.
Mbunge
wa Jimbo la Sikonge Ndugu Said Mkumba akihutubia wakazi wa Tabora mjini
na kutaka sheria zianze kufuatwa kwa viongozi wa siasa kutojishirikisha
na vyama vya ushirika.
Mbunge
wa Viti Maalum Ndugu Ummy Mwalimu akiwasalimu wakazi wa Tabora mjini na
kuwaambia wakina Mama wa Tabora umuhimu wa kujiendeleza katika kuleta
maendeleo na umuhimu pia wa Muungano wetu kati Tanzania Bara na
Zanzibar.
Mbunge
wa Jimbo Mtera Joseph Lusinde akiwahutubia wakazi wa Tabora kwenye
mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM uliofanyika kwenye stendi ya
mabasi ya zamani ambapo aliwaambia wana CCm tusioneane aibu kama mtu
amekosea achukuliwe hatua mara moja .
Matukio yakienda live kwa kupitia simu.
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Amos Makalla (Mb) akihutubia wakazi wa Tabora
ambapo aliwaeleza mipango ya muda mfupi na mipango ya muda mrefu ya
kutatua matatizo ya maji mkoani hapo.
Mmoja
wa Wazee waasisi wa CCM Tabora akipiga picha ya ukumbusho kwenye
mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
uliofanyika kwenye stendi ya mabasi ya zamani.
Mbunge
wa Urambo Mhe. Samuel Sitta akiwasalimia wakazi wa Tabora mjini kwenye
mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kuwasili
kwenye uwanja wa mkutano stendi ya mabasi ya zamani,Tabora mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa CCM wakitembea
kuelekea eneo la mkutano baada ya kula chakula cha mchana kwa wakina
mama lishe wa stendi mpya ya mabasi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula kwa Mama Lishe wa
stendi mpya ya mabasi Tabora pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma
Mwassa kabla ya kuelekea kwenye mkutano wa hadhara kwenye stendi ya
mabasi ya zamani ,Tabora mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila chakula cha Mama lishe wa
Tabora mjini stendi mpya ya mabasi kabla ya kwenda kwenye mkutano wa
hadhara,kulia kwake ni Mbunge wa Viti Maalum Munde Tambwe na Mbunge wa
Tabora mjini Ndugu Ismail Aden Rage.
KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI TABORA
Reviewed by
uhurutz
on
16:20
Rating:
5
No comments: