TAARIFA KUHUSU BOMU LILILOONEKANA MTWARA


Hili
ni bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha Mdui kata ya
Mawala wilaya ya Mtwara vijijini kwenye mkoa wa mtwara liliokotwa na
watoto waliokua wakicheza karibu na eneo la makaburi.Taarifa ilitolewa
Polisi baadae ambapo baada ya wataalamu kuja na kuchunguza waligundua ni
bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT
SOL 618 ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi walichukua
hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.
Kaimu
kamanda wa Polisi Mtwara Maisha Maganga ameongea na na kusema
‘ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu nadhani ni kipindi kile
cha vita ya Msumbiji, tulilipeleka porini likalipuliwa na ulipuaji wake
haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema limeletwa ama
imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu’


Baadhi ya maaofisa kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania wakitazama bomu hilo
No comments: