Dk Titus Kamani: Nitakufa na wetendaji watakaochakachua Fedha za mirdi ya maji
Dk Titus Kamani akikagua mradi wa maji jimbo la Busega
Na Antony Sollo Busega
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, amewaonya watendaji
watakaotafuna fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa jimbo la Busega.
Dk. Kamani, alitoa kauli hiyo jana
akikagua mradi wa maji katika kijiji cha Nyangili Kata ya Igalukilo jimbo la
Busega Mkoani Simiyu ambapo pamoja na mambo mengine Dk Kamani alikagua miradi
mbalimbali inayotekelezwa katika Kata hiyo.
Alisema,mradi huo umetumia fedha nyingi ambazo wala si bajeti ya Serikali
bali ni juhudi zake binafsi kama mwakilishi wa wananchi hao lakini
akiwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Marafiki ,wahisani pamoja na Benki ya
Dunia, “nawaomba ndugu zangu muulinde
mradi huu na kuhakikisha wananchi
wanahudumiwa bila kubaguliwa”
Mradi wa maji katika kijiji cha Nyangili Kata ya Igalukilo jimbo la Busega
Mkoani Simiyu umetumia kiasi cha shilingi milioni 300,000,000.ikiwa ni fedha
kutoka Benki ya Dunia.
Najua mmepata shida hii ya maji kwa muda mrefu hatimaye serikali yenu
imesikia kilio chenu, hivyo kuuharibu au kuuchakachua mradi huu ni kutaka muendelee
na shida iliyokuwa inawasumbua na ninaapa,nitakufa na watu watakaofuja fedha za
miradi inayotekelezwa katika jimbo letu.
Dk Kamani ameitaja miradi inayotekelezwa katika kata ya Igalukilo kuwa ni pamoja na mradi wa Umeme unapita katika kijiji
cha Nyangili,Lunala na Mwamagigisi,na mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa
Kituo cha Afya Igalukilo.
Upande wa ujenzi wa barabara,Dk Kamani alisema kuwa miradi ya barabara
imetengewa shilingi milioni 300,000,000. Ambapo alisema barabara ya Mwamjulila
na badugu itatengenezwa na itapitika kwa urahisi kuliko ilivyokuwa hapo awali
kabla ya Uongozi wa Dk Kamani.
Baada ya kukagua miradi mbalimbali katika kata hiyo Dk Kamani alihutubia
Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Malangale ambapo aliwashukuru wananchi wa
kata hiyo kwa kumpigia kura na kumpa ushindi na kuwaahidi kuwa ataendelea
kutimiza ahadi pamoja na kutekeleza ilani ya chama kwa kuwaletea maendeleo ya
pamoja,badala ya kushughulika na mtu mmoja mmoja.
Dk Kamani aliguswa na Risala ya kikundi cha wananchi kinachojulikana kama
fogong’ho ambacho kinafanya shughuli za kuchangiana na kukopeshana fedha kwa
ajili ya kujinunulia mahitaji madogomadogo ambapo alitoa mchango wa shilingi
laki tano500,000. kuunga mkono juhudi za wanakikundi hao.
Akihitimisha hotuba yake,Dk Kamani alitoa mpira kwa wachezaji wa timu ya
Zege Malangale FC na kuwaasa kuwa,michezo ni Afya hivyo ili waweze kuwa na Afya
njema wajitahidi kushiriki Michezo mbalimbali ikiwemo mpira wamiguu,riadha,mbio
za baiskeli na michezo mingine ili kuzilinda Afya zo.
Akizungumzia watu wanaopita kufanya kampeni chafu jimboni Dk Kamani
alisema,ndugu zangu wananchi wa Malangale, kuweni macho na watu wanaopita
kuwarubuni,maendeleo hayatapatikana kwa kugawiwa fedha kwa mtu mmoja mmoja bali
nawashauri kuwa fursa ziko nyingi hebu undeni vikundi vya ushirika ili Serikali
iweze kuwapa ruzuku katika shughuli za Uvuvi.
“Serikali kwa sasa inatoa ruzuku ya asilimia arobaini ( 40 ) kwa
wanaushirika wa vikundi vya Uvuvi ili ziwasaidie kununua mitumbwi na Nyavu kwa
ajili ya shughuli za Uvuvi changamkieni fursa hii kwani mimi niko tayari
kuwaonyesha njia ili muweze kunufaika na sekta hii ambayo iko katika eneo lenu.alisema
Dk Kamani.
No comments: