Ads Top

MASHABIKI WA BRAZIL WAOMWA RADHI

Ni baada ya kupigwa 7- 1 na Ujerumani

By Admin 
Beki na nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Brazil, David Luiz Moreira Marinho, amewataka radhi mashabiki wa soka wa nchi hiyo kufuatia kisago cha mabao saba kwa moja walichokipokea kutoka kwa Ujerumani usiku wa kumaki hii leo huko Estádio Mineirão, mjini Belo Horizonte.
Luiz, ambaye alichukua jukumu la kukiongoza kikosi cha Brazil kufuatia nahodha Thiago Silva, kutumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi mbili za njano, amesema mpaka sasa hawajui nini kilichosababisha kupokea kisago hicho ambacho kinaiingiza nchi hiyo katika rekodi mpya kwenye medani ya soka duniani.
Amesema wanatambua mashabiki wa soka nchini humo, wameumizwa mon na kichapo hicho, lakini akasisitiza hawana budi kusamehewa na kuendeleza umoja waliokuwa nao kama walivyoanza fainali za kombe la dunia za mwaka huu June 12.
Kwa upande wa mlinda mlango wa Brazil, Julio Cesar amesema soka lina maajabu yake na usiku wa kuamkia hii leo, maajabu ya hatari yaliwageukia wao kama wenyeji, hivyo hawana budi kukubaliana na hili hiyo.
Timu ya taifa ya Brazil imekubali kufungwa mabao saba kwa moja na kuwa timu ya kwanza duniani kufungwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia.
Mabao ya Ujerumani katika mchezo huo yalipachikwa wavuni na Thomas Müller, Miroslav Klose, Sami Khedira, Toni Kroos aliefunga mabao mawili pamoja na André Horst Schürrle aliefunga mabao mawili pia

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.