Mfanyakazi wa Mzani wa Usagara ahojiwa na Takukuru kwa saa saba
· Ni kwa tuhuma za kuomba
na kupokea Rushwa
Na Antony Sollo Mwanza.
August 5.2014.
MFANYAKAZI
wa Mzani wa Usagara Jijini Mwanza,Yusuf Kasumula amehojiwa kwa zaidi ya saa
saba na Maafisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU,akituhumiwa
kuomba na kupokea Rushwa akiwa kazini imefahamika.
Tukio
hilo lilitokea August 2 mwaka huu majira ya saa 4 : 00 Asubuhi katika eneo la
Usagara Mzani wa Usagara baada ya Photidas Kennedy ( 40 ) Dereva wa gari namba za
usajili T 864 CGD aina ya Fusso lililokamatwa usiku wa terehe 02 August 2014
saa 4:00 usiku na kuombwa Rushwa ya shilingi laki moja,akidaiwa kuzidisha uzito
wa mzigo katika gari lake.
Imedaiwa
kuwa mtumishi wa Mzani wa Usagara Yusuf Kasumula aliomba kiasi hicho cha fedha ili
amuachilie Kennedy aendelee na safari yake jambo ambalo Kennedy alilipinga
vikali.
Baada ya kusumbuliwa muda
mrefu Kennedy alilazimika kutoa kiasi hicho cha fedha shilingi 75,000 na kumpa Kasumula na baada ya hapo Kennedy
aliomba msaada kwa Maofisa wa Takukuru.
Tukio hilo liliripotiwa kwa
mwandishi wa habari wa gazeti hili ambaye alishirikiana na Kennedy kutafuta
ufumbuzi wa tukio hilo ambapo kwa pamoja walitoa taarifa kwa Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza Christopher Cyprian Foime
ambaye aliwasiliana na Uongozi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa Mkoa wa Mwanza.
Kamanda wa Takukuru Mkoa
Mwanza aliwajulisha Maafisa wa Taasisi hiyo Wilaya ya Misungwi Julian Augustine
wakiwa na Dereva Bahati Nzumbi walifika Usagara na kufanya mahojiano na Yusuf
Kasumula.
Wakizungumza na Tanzania Daima
baadhi ya Madereva wanaotumia Mzani huo kutoka Mikoa mbalimbali nchini ,wamelalamikia
kitendo cha kupima katika Mizani ya Mikoa mingine na Uzito wa Mizigo yao kuwa
sahihi,lakini wanapofika katika Mzani huo uzito wa Mizigo yao hubadilika na
matokeo yake kuombwa rushwa na wakikataa kutoa rushwa hupigwa faini kwa lengo
la kukomolewa.
Madereva waliopatwa na mkasa
huo ni Khasim Hausi dereva wa Lori lenye namba za Usajili T 210 CAQ aina ya
Fusso.
Khasimu ameliambia Tanzania Daima kuwa wakati
anatoka Karagwe na kupima Mzani wa Kyaka mzigo wake ulikuwa na Kilo 6000 mbele
na upande wa nyuma ilikuwa ni kilo 9800.
Khasim amedai kuwa alipofika
Mzani wa Usagara Mzigo wake ulipimwa na kuonyesha kuwa ulikuwa umezidi kilo 250
jambo ambalo hakukubaliana nalo maana hakuongeza mzigo wa aina yoyote njiani.
Baadaye Khasim aliombwa atoe
fedha kiasi ambacho ni kikubwa na akalalamikia unyanyasaji wanaofanyiwa
Madereva wanaotoka Mikoa mbalimbali nchini na watendaji wa Wakala wa Barabara
TANROADS Mkoa wa Mwanza.
Baada ya kufuatwa na waandishi
wa habari na kuhojiwa kuhusiana na madai ya Khasim na Kennedy Kasumula alikiri
kuwafahamu Madereva hao na kusema kuwa Magari yao yalizidisha uzito.
Kuhusu kulipa faini na
kushindwa kupewa risiti Kasumula alisema kuwa “taratibu za Ofisi ya TANROADS
unalipa kwanza na risiti utapewa baada ya mzigo wako kukaa vizuri.”
Katika kile kinachodaiwa
kuwatisha Maafisa wa Takukuru,mzani wa Usagara unasoma nyaraka zake tofauti na
sehemu zingine kwa kuwa iwapo utapima mzigo wako hapo tarehe 5 August mwaka huu
nyaraka zako zitaonyesha ulipima tarehe 6 August jambo ambalo madereva na wadau
mbalimbali wamedai kuwa iwapo kuna makosa katika usomaji wa tarehe basi kuna
mashaka makubwa hata katika upimaji wa uzito wa mizigo.
Uchunguzi
uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa,kuna dalili za wizi na ubadhilifu
mkubwa unaofanyika katika Mzani wa Usagara kwani hata usomaji wa nyaraka katika
mzani huo hauendani na uhalisia.
Akizungumzia utata wa kusoma
tarehe ya siku inayofuata badala ya tarehe husika Mhandisi wa Tanroads Mkoa wa
Mwanza Pius Joseph aliliambia Tanzania Daima kuwa ni kweli kuna tatizo la
usomaji wa tarehe katika mzani huo.
“Ni kweli kuna tatizo la
kusoma kwa tarehe katika mzani huo tunalifahamu ni la muda
mrefu,tutalishughulikia.”alisema Joseph.
Kukiri kwa Mhandisi huyo juu
ya utata katika kusoma kwa tarehe kumethibitisha madai ya kuchakachuliwa kwa
Mzani wa Usagara.
Wakizungumzia kwa uchungu
dhidi ya uonevu wanaofanyiwa na watendaji wa Mzani wa Usagara Madereva
mbalimbali wanaotumia Mzani wa Usagara wameiomba Serikali ishughulikie tatizo
hilo kabla hawajatangaza mgogoro mkubwa ambapo walisema ifikapo Augosti 15
wataanza mgomo utakaoendeshwa bila kikomo kwa kuweka magari kuzuia huduma ya
Usafiri wa aina yoyote kwa barabara ya Usagara Misungwi ,Kigongoferry na
Sengerema.
Maafisa hao wa Takukuru walichukua takribani
masaa saba kuchukua maelezo ya na Yusuf na baada ya mahojiano hayo,waliondoka na
nyaraka mbalimbali zinazotumika katika Mzani uo kwa uchunguzi.
No comments: