Waziri wa afya nchini Nigeria amethibitisha visa kumi vya ugonjwa wa Ebola

Idadi ya waliofariki kutokana na Ebola yazidi kuongezeka Afrika Magharibi
Waziri wa afya nchini Nigeria amethibitisha visa kumi vya ugonjwa wa Ebola.
Wagonjwa wote walishikana na raia wa Liberia ambaye alizimia alipowasili katika uwanja wa ndege nchini humo na kufariki baadaye.
Bwana Chukwu amesema kuwa kisa cha hivi karibuni ni kile cha muuguzi aliyemtibu mgonjwa huyo.
Mjini Geneva Shirika la afya duniani linafanya mkutano wa wataalam wa matibabu ili kujaribu utumizi wa matibabu mapya.Watajaribu kutumia dawa ambazo hazijatumiwa na binaadamu.
No comments: