Ads Top

Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Akaribishwa Rasmi Wizara ya Katiba na Sheria

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (kushoto) akikaribishwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa shada la maua kutoka kwa mtumishi wa Wizara Bi. Christina Jenga jana (Jumatano, Januari 7, 2015) jijini Dar es Salaam huku Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Maimuna Tarishi akishuhudia. Bw. Masaju alifika Wizarani kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete ili kubadilishana mawazo na viongozi na watumishi wa Wizara.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju akipokewa na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jana(Jumatano, Januari 7, 2015) wakati alipofika Wizarani hapo kukutana na viongozi na watumishi ili kubadilishana mawazo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro jana(Jumatano, Januari 7, 2015) wakati alipofika Wizarani kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais jakaya Kikwete hivi karibuni. 

Na Mwandishi Wetu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju amewakumbusha watumishi wa umma katika sekta ya sheria kufanya kazi kwa ushirikiano na uzalendo ili kulinda maslahi ya taifa.

Bw. Masaju, ambaye ameteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo, amefafanua kuwa watumishi wa umma wanapozingatia uzalendo katika utendaji wao, wanapata nguvu ya kusimama na kukemea maovu.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.