MOTO WATEKETEZA JENGO LA POSTA ENEO LA SOKO LA SABASABA MANISPAA YA DODOMA.


Moto
mkubwa umezuka na kuteketeza jengo la posta ndogo lililopo eneo la soko
la sabasaba manispaa ya Dodoma huku vitu nyote viliyokuweno ndani ya
jengo hilo vikiungua ambapo gharama halisi na hasara ikishindwa
kufahamika mara moja.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ya moto wanadai chanzo ni
hitilafu ya umeme iliyojitokeza katika jengo hilo na kusababisha baadhi
ya maeneo kushika moto ambao ulisambaa kwa kasi na kuteketeza mali na
thamani zilizokuwemo ndani yake.
Akizungumzia ajali hiyo meneja wa posta mkoa wa Dodoma Magreth
Ulyomi amesema alipata taarifa kutoka kwa mmoja kati ya wafanyakazi wa
ofisi hyo kuwa kuna cheche za moto zinaonekana katika jengo hilo kabla
ya kuwaka na kuteketea.
Awali muda mfupi baada ya kuzuka kwa moto huo jeshi la zimamoto na
uokoaji mkoa wa Dodoma lilifika lakini lilishindwa kuingia kwenye eneo
la tukio kutokana na ujenzi holela wa vibanda vya wafanyabiashara sokoni
hapo hali iliyochangia mapambano dhidi ya moto huo kushindwa kufanyika
kwa ufanisi.
No comments: