WATU 7 WAMEFARIKI NA WENGINE ZAIDI YA 56 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI BASI MKOANI MARA.

Watu
saba wamafariki wamefariki dunia na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa
vibaya baada ya basi la abiria la nata raha yenye namba za usajili T 473
CJN linalofanya safari zake kati ya Mugumu wilayani serengeti kupitia
Bunda kwenda mkoani Mara kupalamia nyumba eneo la njia nne mjini Bunda
baada ya breki za basi hilo kukatika likiwa katika mteremko mkali.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda Bw Joshua
Mirumbe, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bunda, akizungumza baada ya
kufika eneo la tukio, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa
tano asbuhi na kusema kati ya majeruhi hao wanane wamepelekwa hospitali
ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza huku wengine wakilazwa hospitali
teule ya DDH mjini Bunda.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamedai baada ya kukaribia njia
kuu ya Mwanza Musoma mita chache tu kufika kituo kikuu cha mabasi
mjiniBunda mwendo wa basi hilo uliongezeka na baada ya kuhoji walielezwa
kuhusu kukatika kwa breki hizo kabla ya kuvamia jengo hilo.
Hata hivyo wakati mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama
akisema walifariki ni abiria saba lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mara
ACP Philip Alex Kalangi akizungumza na ITV kwa njia ya simu amesema
abiria sita ndiyo waliofariki katika ajali hiyo.
chanzo ITV
No comments: