Ads Top

EMIRATES YAONGEZA MUDA WA NAULI MAALUM ZA DUBAI NA OFA YA VIZA BURE. OFA HIYO PIA KUJUMUISHA USIMAMIZI WA MIZIGO NA MY EMIRATES PASS



DAR ES SALAAM, TANZANIA, 12 JULY 2017, Emirates imeongeza muda wa ofa kwa wasafiri kutoka Tanzania kwenda Dubai kwa ofa maalum ndani ya daraja la kawaida na daraja la juu kwenye nauli ya kwenda na kurudi ambayo itaambatana na viza bure, nafasi ya kuweka mzigo usiozidi kilo 23 na My Emirates Pass.
 

Ndani ya ofa hii maalum, Tiketi ya daraja la kawaida kutoka Dar Es Salaam mpaka Dubai ni USD 399 na daraja la juu ni USD 1999. Ofa hiyo ya nauli inatengemea na uwepo wa nafasi, vigezo na masharti na kwa muda ulioainishwa tu. Unaweza kutuma maombi ya kupata nafasi kati ya 11 Julai na 24 Julai wakati safari ni kati ya 11 Julai na 30 Novemba 2017. Gharama ya tiketi inajumuishwa pia na kodi ya uwanja wa ndege.


Ikipigiwa kura na wasafiri kuwa chombo maridhawa kwa kutoa huduma duniani mwaka 2017 katika kinyanganyiro cha TripAdvisor Travelers' Choice Awards. Emirates pia inatoa ofa ya viza ya siku 30 ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (inatengemea na uthibitisho wa idara ya uhamiaji), nafasi ya kuhifadhi mzigo isiozidi kilo 23 kwa daraja la kawaida na mpaka kilo 32 kwa daraja la juu, vile vile My Emirates Pass inaweza kutumika kwa ofa mbalimbali na kupata punguzo ndani ya Dubai.


My Emirates Pass ambayo inatumika mpaka 31 August 2017, inawapa wateja punguzo maalum katika mahotel na migahawa zaidi ya 120 yenye ubora duniani ndani ya Dubai. Pia kuna ofa mbalimbali katika nyanja ya burudani, kutembelea shindano la gofu, kutembelea mbuga na sehemu maridhawa ndani ya jiji la Dubai. Kuona ofa za My Emirates Pass tembelea www.emirates.com/english/offers/4221290/my-emirates-pass


Ukiwa Dubai kwenye mandhari tulivu, utafanya manunuzi ya vitu vya hali ya kimataifa, kupata huduma kwenye migahawa mikubwa, kupunga upepo kwenye fukwe tulivu na kuona majengo ya kila aina, Dubai inakupa ladha ya kifamilia. Wageni wakiwa huko wanaweza kutumia My Emirates Pass kufurahia vivutio vya jiji na sehemu maarufu kama Hifadhi ya Dubai na mwambao ikiwemo na hifadhi tatu maarufu kama bollywood, Dubai Motiongate bila kusahau hifadhi ya kwanza katika mkoa huu legoland park na legoland water park.


Jiji la Dubai pia ina ofa ya malazi inayoendana na matumizi yako.


Katika kila ndege za Emirates wasafiri watapata viburudisho vya program za television katika chaneli 2500 kutokana na mahitaji yao ikiwemo ya kusikiliza na kuona kutoka sinema mpya, muziki na michezo, pia bidhaa rafiki za kifamilia na huduma kwa watoto kama michezo, chakula kwa watoto na sinema, kupewa kipaumbele kama familia na matumizi ya bure ya kubebewa mzigo ndani ya uwanja wa Kimataifa wa ndege ya Dubai.


Kwa kuongezea, ili kupata utulivu wa kujihami na bidhaa, wateja watapata ukarimu wa kimataifa toka kwa wahudumu wa kimataifa kutoka kwenye safu yetu huku wakiburudika kwa vyakula vilivyoandaliwa kitaifa na kimataifa na wapishi wetu kwa kutumia vyakula asili ikizindikizwa na aina mbalimbali ya vinywaji


Emirates inasafiri mara moja kila siku kati ya Dubai na Dar Es Salaam ikitumia Boeing 777. Kupata nafasi au kwa maelezo mengine kuhusu tiketi, vigezo na masharti tafadhali tembelea www.emirates.com/tz, ofisi za Emirates au mawakala wa Emirates.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.