Ads Top

MAFISANGO AFARIKI DUNIA


TANZANIA imepoteza mchezaji mwenye uwezo wa juu, Patrick Mafisango, licha ya kwamba hakuwa Mtanzania lakini mchango wake kwenye soka la nchi hii utakumbukwa miaka mingi ijayo.
Mafisango ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari, alikuwa ni mmoja ya wachezaji wenye uwezo mzuri wa kucheza nafasi ya kiungo na ulinzi. Pamoja na kwamba alikuwa na udhaifu wake, bado jopo la ufundi lilitambua mchango wake na ndiyo maana liliendelea kumtumia.
Kabla ya kufikwa na umauti, Mafisango ambaye ni mzaliwa wa DR Congo lakini akiwa na uraia wa Rwanda, aliwahi kucheza katika klabu ya Azam kisha kutua Simba. Global Publishers & General Enterprises Ltd, tunatoa pole kwa familia ya marehemu, klabu ya Simba, mashabiki wa soka na wadau wengine wote walioguswa na msiba huyo.
Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Imetolewa na:
GPL

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.