Ads Top

JINSI YA KUJIUNGA NA INTERNET KWENYE SIMU YA MKONONI

Kwa mitandao ya VODACOM,ZAIN na TIGO.
Mtandao wa Vodacom
Nenda sehemu ya kuandikia message halafu Andika neno
INTERNET
acha nafasi na andika aina yako ya simu, mfano:
NOKIA 6030,6030b,2626,6060 n.k
Halafu tuma kwenda namba 15300.. Utaletewa ujumbe mfupi. Usemao Internet setting will be sent to......subiri kidogo mpaka message ya pili ije halafu utaingiza namba za siri au PIN ambazo ni 1234 halafu SAVE hizo setting... Utakuwa umejiunga na internet tayari..kwahiyo utakuwa na uwezo wa kudownload NYIMBO,PICHA,VIDEOS kulingana na uwezo wa simu yako.
Kwa Mtandao wa Airtel
Kwa mtandao wa Airtel andika neno: WAP halafu tuma kwenda namba: 232
Kwa mtandao wa Zain hauitajiki kutuma aina ya simu yako, bali andika neno WAP tu halafu tuma kwenye namba 232..Utaletewa ujumbe wa kukubaliana na Setting za internet na fuata maelezo mengine.
Kwa mtandao wa TIGO
Kwa mtandao wa TIGO..andika neno WAP acha nafasi halafu andika aina yako ya simu
Mf: NOKIA 6030,6030b,N90,N73 n.k
Halafu tuma kwenda Namba: 500
Halafu fuata maelekezo utakayopewa baada ya kutuma message hiyo.

KAMA NJIA HIYO HAPO JUU IMESHINDIKANA JARIBU NA HII HAPA CHINI
 Simu za kichina ni simu nzuri sana japo zina mapungufu mengi ila pia zina faida kem kem..Kuunganisha internet kwenye mchina wako ni rafisi sana Haina haja ya kwenda ofisi za tigo wala voda wala nini, Tuliza kichwa chini na ufatishe haya maelekezo hatua kwa hatua. VITU VYA KUZINGATIA 1. APN : Internet or wap 2. Home page: www.mlimakilimanjarotz.blogspot.com 3. Proxy adress: 010.111.033.243/ 010.154.000.008(Au angalia kwenyesimu iliyokubali internet) 4. Proxy port: 8080 / 9401 Kumbuka kuwa Baadhi ya mitandao huwa inaingiliana proxy,so ukiseti hizi unaweza weka line yoyote na ikakubali,ila zingine hazikubali hadi ujue proxy zake. kufahamu tafuta simu ambayo imeunganishwa tayari,nenda kwenye setingi na utafute mwenyewe SASA FATA HATUA KWA HATUA.KWANZA TUBADILISHE Data Account. FANYA HIVI ;- 1. Bonyeza Services => Data account => GPRS 2. Bonyeza profile yoyote na Bonyeza “edit profile” 3. Ipe jina hiyo profile. (mfano: kwa tigo andika “TIGO” AU VODA ) 4. Andika APN (internet) 5. Sehemu ya username na password USIJAZE KITU na authentication weka normal 6. Sasa save profile yako na iactivate HATUA YA PILI NI KUSET GPRS setting kwa kutumia Data account ya hapo juu. FANYA HIVI ;- 1. Nenda kwenye Services 
=> WAP =>Settings=>Edit profile 2. Bonyeza profile yoyote na Bonyeza “edit profile” 3. Ipe jina hiyo profile. (mfano: kwa tigo andika “TIGO”) 4. Ipe mtandao (www.google.com) 5. Kwenye Data account select Ile tuliyo iseti kwenye hatua ya kwanza 6. Kwenye connection type chagua HTTP na ipe ile proxy adress na proxy port 7. Sasa save na activate 8. Tayari sasa waweza ku surf web, gprs umesha iactivated kwenye mChina mobile yako Huu ni mfano kwa tigo tu. Fatisha maelekezo haya kwa mitandao mingine pia. Nitaendelea kuwapatia Proxy adress za mitandao mingine kwa ajili ya mchina mobile yako. Endelea kusubiri


KWA WALE WANAO TUMIA SIMU ZENYE ADROID 
fungua kwenye seting nenda kwenye Wi-Fi fungua mobile data au mobile networks ukisha fungua hapo nenda kwenye acess point names 
add new APN  
name tigo Tanzania,airtel tz, vodacom, tanzania
APN weka Internet 
proxy usiandike kitu 
port unaweza kuweka 8080 au ukaacha wazi 
authentication type weka none
APN protocal weka IPv4  
kisha save seting yako  

1 comment:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.