Ads Top

TPF5 fainali ni leo Nani kubamba 90m?

 
 Baadhi ya washiriki wa TPF5 wakiwa katika picha ya pamoja
Kupitia kituo cha Televisheni cha Star TV leo na kesho macho ya mashabiki wa muziki yako pima kuangalia ni nani atachukua nadasi ya Davis katika kinyang'anyiro cha kumtafuta nyota wa muziki anayechipukia, shindano linaloletwa kwa hisani ya Bia ya Tusker huu ukiwa ni mwaka wa tano.
Linaitwa Tusker Project Fame na huu ni msimu wa 5, hii ni wiki ya nane ambapo washiriki kutoka jumla ya nchi sita wamekuwa wakichuana huku wengine wakiwa wanajifunza mambo mbali mbali katika jumla la mafunzo ya sanaa, ya muziki lililopachikwa jina la Tusker Academy.
Zawadi ya Miliono 90 imekuwa kama kubwa hivi kulinganisha na kiwango cha mwaka jana, huku washiriki wa nchi za Tanzania, Uganda na Southern Sudan wakionekana kutolewa siku za mwanzoni kabisa.
Ukilinganisha na msimu uliopita, Tanzania ilikuwa mbele kabisa huku bendera ikipeperushwa na Peter Msechu, mpaka siku ya mwisho ambapo pengine isingekuwa alama kidogo za juu za Davis Ntare, tungekuwa tunaongelea mengine.
Imani Lissu na Damian Mihayo hawakuweza kufua dafu kwenye jumba hilo, na hivyo tanzania ilipotea mapema kabisa kwenye mashindano haya yanayotajwa kuwa na mvuto kuliko shindano lolote la kusaka vipaji vya uim,baji Afrika ya Mashariki na kati.
Kufuatia kutoka kwa washiriki mbali mbali, mchi ambazo zimeachwa kuwania taji ni tatu tu Kenya ambao ni wenyeji, ambao wana washiriki watatu, Rwanda na Burundi.
Ruth, Doreen and Steve wataiwakilisha Kenya, Jackson ataiwakilisha Uganda na Joe ataiwakilisha Burundi kwenye fainali za Kesho.
Majaji, wanajulikana kwa busara zao na wengine sasa kama Ian Mbugua ametoka kuitwa Jaji mkatili mpaka kuwa burudani kwa mashabiki wa shindano hili, yeye anatokea Kenya lakini kwa tanzania pia tuna Hermes Bariki na kutoka Uganda, kuna Juliana Kanyomozi ambaye ni mwanamuziki.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.