Ads Top

WANACHAMA WA CCM KISHAPU


                                        
                                                          WANACHAMA NA WAKEREKETWA  WA CCM
                                                          S L P  1288                     
                                                          MHUNZE- KISHAPU
                                                          SHINYANGA.
                                                          25/ AUGUST/ 2012
                                                                                                       

KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI,
WILAYA YA KISHAPU,
S L P 77,
KISHAPU,
SHINYANGA.

YAH: HUJUMA ZINAZOFANYWA NA MBUNGE WA JIMBO LA KISHAPU JUU YA CHAGUZI ZA CHAMA NA JUMUIYA MBALIMBALI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Ndugu ,
Rejea kichwa cha habari hapo juu chaelezea,
Sisi wanachama ,wapenzi na wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi kupitia jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, tunapenda kuleta Malalamiko juu ya hujuma wanazofanyiwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi zoezi linalofanyika nchi nzima kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Chama chetu.

 Tumesikitishwa na jinsi mwenendo wa Mbunge huyu kuanza kujiingiza katika s
uala hili muhimu kwa mustakabali wa chama chetu kuamua kufanya 
mambo mbalimbali yanayopelekea kukiua Chama ambapo kwa baadaye lawama 
zitakwenda kwa wananchi kuonekana kukiasi chama bila kuelewa kiini cha Uasi huo,
Kwa mantiki hiyo sisi kama wanachama makini tunaokitakia mema chama tumeona 
tufichue hujuma hizi mapema ili hata kama Chama kitakapokuja kukosa imani na 
 wanachama pamoja na wananchi  kuamua kuhamia upinzani ieleweke kwamba, 
aliyepelekea yote haya ni Mbunge wa Jimbo la kishapu Bwana Suleiman Masoud 
Nchambi. 
Hujuma za wazi zinazofanywa tena bila kificho ni hizi hapa!
1.Ni mkakati wa kupanga safu ya kamati ya Siasa ya 
Wilaya itakayokuwa 
chini ya mamlaka yake.
2. Mpango mkakati wa kuhamishwa kwa baadhi ya viongozi ambao   
 wanamsimamo tofauti na matakwa yake.
3. Kuwakusanya viongozi wa Jumuiya zote za chama na na viongozi   
kuwapeleka shambani kwake na sehemu zingine kwenda kuweka msimamo 
wa nani awe kiongozi wa jumuiya Fulani hususani wenyeviti wa Jumuiya na 
viongozi wa chama.
4.Ni juu ya Ushirika alio nao kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Wilaya na Mkoa ili imwachie uwanja mpana wa kucheza Rafu hizi jambo ambalo limekuwa ni kawaida kwa Taasisi hiyo hususani chaguzi mbalimbali na hata uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo sasa yanajirudia tena

 5. Mkakati wa kurudishwa kwa viongozi  wasiotakiwa na wananchi waliomsaidia kuhujumu uchaguzi mwaka 2010 ambao tayari wamerudi, jambo linaloendelea kulalamikiwa na wananchi pamoja na wanachama lakini hawana wa kuwasikiliza.
6. Mbunge huyu kuendeleza makundi ndani ya chama kabla na baada ya chaguzi kwa kutotaka kuvunja kambi na sasa anapelekea kuwa mmiliki wa chama chetu jambo ambalo halikubaliki.
Ufafanuzi wa juu ya Hujuma hizo ni kama ifuatavyo:
1.Ni mkakati wa kupanga safu ya kamati ya Siasa ya Wilaya itakayokuwa chini ya mamlaka yake:
Mkakati huu ni kwamba Mbunge anapandikiza mtu anayemtaka na kugharimia fedha usafiri chakula na malazi kwa wajumbe wanaokwenda kupiga kura na hivyo kufanya uchaguzi kuwa si huru na wa Haki jambo linalokemewa vikali na viongozi wa chama chetu ngazi za juu.
2.Mpango mkakati wa kuhamishwa kwa baadhi ya viongozi ambao wanamsimamo tofauti na matakwa yake:
Suala hili limejitokeza mara nyingi ambapo ipo mifano  hai ya viongozi waliohamishwa kwa matakwa ya Mbunge.
Waliohamishwa kwa matakwa ya Mbunge huyo ni pamoja na Katibu aliyekuwa na msimamo tofauti na Mbunge huyo na ambaye alikuwa ni tumaini jipya kwa wana chama wa CCM jimbo na  Wilaya ya Kishapu ambaye kwa sasa yupo wilaya ambayo hatutaitaja kwa sababu za kiusalama na Katibu wa UVCCM ambaye naye alinyanyaswa kwa kusimamishwa na hatimaye kupewa uhamisho kwenda Wilaya pia ambayo nayo hatutaitaja kwa sababu maalumu za kiusalama.

 Lakini pia hakuna atakayepinga wala atakayezuia hisia za wapiga kura wa jimbo la Kishapu juu ya hujuma alizofanyiwa Mbunge wa jimbo la Kishapu kipindi cha awamu ya 2005/2010 na kupelekea kuachia ngazi na huyu tunamtaja kwa vile tukio hili halijawahi kutokea katika Dunia nzima kwa mtu kufanyiwa hujuma iliyokuwa inapelekea kutofanya hata mikutano na wananchi kwa vile Mjumbe wa NEC ambaye ni mbunge kwa sasa alikuwa akimhujumu Mbunge wa Awamu hiyo kwa kumvurugia mikutano yake akiwatumia watu ambao hata sasa ametumia nguvu za ziada kuhakikisha wanachukua nafasi za uongozi kwa kutumia  fimbo ya fedha zake ambapo Mbunge huyo  ni Bwana FREDY MPENDAZOE
kwa watu ambao hawaijui vizuri historia ya Mbunge wa sasa Bwana Suleiman Nchambi hawatajua kilichopelekea kupata ubunge alio nao ila kwa sasa sisi wanachama na wakereketwa tumeamua kuweka hadharani mambo yote haya kuondoa dukuduku walizonazo wananchi ili viongozi waone hujuma zinazopelekea kuuwa Chama chetu na wakati wananchi wakiwa bado wanakipenda
3.Kuwakusanya viongozi wa Jumuiya zote za chama na kuwapeleka shambani kwake na sehemu zingine kwenda kuweka msimamo wa nani awe kiongozi wa jumuiya Fulani hususani Mwenyekiti wa Jumuiya:
Hili sasa ni janga kwa Chama  chetu cha Mapinduzi kwa vile Serikali ya CCM inazuia kabisa mambo kama haya lakini inashangaza sana kuona kiongozi tena ayeshiriki kwenye chombo cha kutunga Sheria kukiuka kanuni na taratibu za mhimili muhimu kwa Taifa letu,

kwa kuita wajumbe/wapiga kura  na kuwaweka mafichoni kama watumwa kwa lengo la kushinikiza wafanye anachokitaka jambo linaloashiria moja kwa moja rushwa ya bila kificho kwa vile hakuna mtu atakayesafiri umbali zaidi ya kilomita 20 kwa kutumia gharama zake na kuwekwa sehemu bila maslahi fulani, kwa mantiki hiyo kitendo hicho ni Rushwa kabisaaa!!!!
4.Ni juu ya Ushirika alio nao kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Wilaya na Mkoa ili imwachie uwanja mpana wa kucheza Rafu hizi jambo ambalo limekuwa ni kawaida kwa Taasisi hiyo hususani chaguzi mbalimbali na hata uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo sasa yanajirudia tena:
Katika hili,Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya na Mkoa wameshindwa kusimamia majukumu waliyopewa na Mh Rais kwa vile jambo hili Mkoani kwetu siyo geni kwa hiyo viongozi mbalimbali Wilayani Kishapu na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla hawaamini kwamba kiongozi anaweza kupatikana kwa njia ya demokrasia bila kutumia fedha au Maskini naye anayo nafasi ya kuwa kiongozi.
Kwa taarifa hii iwapo viongozi wa kitaifa hamtafuatilia suala hili kwa kuwaondoa makamanda wa TAKUKURU na viongozi mbalimbali wa Chama  na Serikali wanaounga mkono vitendo hivi ieleweke kwamba CCM Kishapu inaondoka kabla ya uchaguzi Mkuu 2015.
5.Mkakati wa kurudishwa kwa viongozi  wasiokubalika na wananchi  na hawa  ndiyo waliomsaidia Mbunge kuhujumu uchaguzi mwaka 2010 na wananchi kukaa kimya kwa kuwa waliamua kukiheshimu chama kwa sasa Hawako tayari kufanyiwa hujuma, kwani Kurudishwa kwa majina ya viongozi hao walioko kwenye mtandao wa Mbunge kwa kutumia fedha zake kupata madaraka hayo ni Ishara ya Anguko kubwa la CCM Kishapu :

 Adolf Hitler aliamini kuwa kiongozi anayechaguliwa na watu wengi si kiongozi lakini kiongozi anayechaguliwa na watu wachache ndiye kiongozi bora suala ambalo hata Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi anavyoamini.
 jambo ambalo kwa sasa ni kinyume na Demokrasia na ni udikteta katika nchi kama Tanzania inayoendeshwa kwa utawala wa Kidemokrasia na uhuru wa kuchagua kiongozi wanayemtaka.
6.Mkakati wa kurudishwa kwa viongozi  wasiotakiwa na wananchi hasa waliomsaidia kuhujumu uchaguzi mwaka 2010 ambao tayari wamerudi, jambo linaloendelea kulalamikiwa na wananchi pamoja na wanachama lakini hawana wa kuwasikiliza.
Chonde Viongozi wetu kipindi hiki tulicho nacho ni tofauti na wakati wowote maana yanahitajika mabadiliko makubwa ya sera na siasa ndani ya Chama chetu kwani kuendelea kumkumbatia mtu ni kukiua chama pasipo na sababu hebu wapeni wananchi uhuru wa kweli wa kumchagua kiongozi wanayemtaka ili kukidhi matakwa ya utawala wa kidemokrasia na kurudisha imani kwa wapiga kura ambao ni wananchi fedha siyo sifa ya kupata kiongozi bora bali kiongozi bora ni Yule aliye chaguo la wananchi pamoja na wanachama wote

 Sisi tunashauri uongozi wa juu wa Chama ushuke kuja kujua namna ya upatikanaji wa viongozi katika jumuiya zote hapa kishapu na sifa zao ili kuondoa mtafaruku unaotarajia kutokea baada ya kukosekana kwa demokrasia ya kweli katika chaguzi hizi.
6. Mbunge huyu kuendeleza makundi ndani ya chama kabla na baada ya chaguzi kwa kutotaka kuvunja kambi na sasa anapelekea kuwa mmiliki wa chama chetu jambo ambalo halikubaliki:
Kwa sasa inavyoonekana Chama cha Mapinduzi ni Moja ya Kampuni zinazoendeshwa na kumilikiwa na Mbunge huyu sasa tunataka tamko juu ya utata huu unaopelekea kukisambaratisha chama chetu:
Je!  CCM ni Kampuni ya Mbunge wa jimbo la Kishapu” au ni Taasisi iliyoanzishwa kwa ajili ya kutetea wanyonge mpaka kuupata uhuru wetu toka kwa wakoloni chini ya uongozi mahiri wa Hayati Baba wa Taifa Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere??
Kama ni Kampuni ya Mbunge tunaomba kutoa msimamo wetu kama wanachama wapenzi,na wakererketwa wa CCM hatuko tayari kuunga mkono katika hilo!!!!!!
Tuna imani kuwa viongozi wetu ni wasikivu mtalifuatilia suala hili kwa karibu na kubaini matatizo yaliyopo katika Wilaya na Kata zetu hapa Kishapu.




Kama Siyo” tunaomba chaguzi zote zisimamishwe ili kutafutiwa ufumbuzi kwa matatizo yaliyopo badala ya kuendeleza mijadala itakayokuja kukimaliza Chama chetu kwani mpaka sasa wajumbe wamepewa msimamo wa watu wanaotakiwa na Mbunge huyo jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya CCM.

 KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Ni sisi wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi-Kishapu
------------------------------------------------------

Nakala:
1.Mwenyekiti wa CCM  Taifa Mh Jakaya Mrisho Kikwete aione kwenye faili lake.
2.Katibu Mkuu wa CCM Taifa kwa taarifa ya ukiukwaji wa maadili ya chama.
3.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa kwa taarifa.
4.Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa kwa taarifa
5.Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ufuatiliaji.
6.Mkurugenzi wa TAKUKURU Edward Hoseah kwa Taarifa
7. Mbunge Jimbo la Kishapu kuondoa dhana ya kuita haya ni Majungu

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.