Ads Top

TAKUKURU YAZINDUKA KISHAPU

MABASI YA KAMPUNI YA MOMBASA RAHA YALIYOKUWA YAKIWABEBA WAJUMBE KUJA KWENYE KITUO CHA KUPIGIA KURA KATIKA CHAGUZI ZA JUMUIYA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KISHAPU SHINYANGA.

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KISHAPU AKIWA NA KATIBU WA CCM MKOA WA SHINYANGA PAMOJA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WA JUMUIYA HIYO KUTOKA MKOANI KUSHOTO NI BWANA MFANGA GURISHA KABLA YA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA UWT

KATIBU MKUU WA CCM MKOA WA SHINYANGA BWANA NGALAWA AKIWA ANAKARIBISHWA RASMI NA M/KITI WA JUMUIYA AMBAYE ALIKUWA NI MGOMBEA WA NAFASI HIYO KABLA YA UCHAGUZI WA JUMUIYA HIYO.

Katibu wa CCM WILAYA YA KISHAPU AKIMSINDIKIZA KATIBU WA CCM MKOA WA SHINYANGA BAADA YA UFUNGUZI WA SHUGHULI ZA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA UWT WILAYA YA KISHAPU.

    Yazuia njama za Kuharibu Uchaguzi zilizopangwa
·              Yaomba wananchi waiamini ipo kwa ajili yao
·               Kambi iliyoratibu mpango wa Rushwa yaumbuka
Na Antony Sollo Kishapu.
Huku kukiwa na maandalizi ya Chaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi na Jumuiaya zake vituko na hujuma zikitisa makundi kwa kuratibu nani awe nani Yaliyojili Wilayani Kishapu yanatia aibu, hii ni kutokana na maandalizi yaliyokuwa na mpango mahsusi wa kupelekea kubadili kanuni za Jumuiya ikiwemo ya namna ya kupiga kura katika makundi ya kata ili zipigwe pembeni na baadaye zikusanywe na kuletwa kwenye sanduku kuu zikitokea pembeni ambapo baadhi ya vijana wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi walisimamia kanuni na hatimaye kuonyesha kuwa wako imara na hawako tayari kuyumbishwa kwa kutumia nguvu ya kundi lenye fedha.
Wakihojiana na mwandishi wa habari hizi Wilayani Kishapu, wanachama wa Chama cha Mapinduzi wamemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi  kwa kuratibu mpango wa kuweka safu itakayokuwa na maslahi kwake huku akitumia fedha ili kufanikisha mpango huo ambapo hata hivyo baada ya vitendo hivyo kukithiri wananchi kwa kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU walifanikiwa kuvikomesha vitendo hivyo na kupelekea uchaguzi wa UWT kuwa huru na Haki tofauti na uchaguzi wa Jumuiya ya UVCCM ambapo mbunge huyo alikuwa akifuatilia kwa karibu kujua nani ataichukua nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo jambo lililopelekea vurugu zilizoamsha hisia za wananchi na wanachama na hatiamaye kutaka kuchoma kwa gari la Mbunge ambapo bila jeshi la polisi kujipanga vizuri na kuonyesha umahiri huenda uchaguzi huo ungeingia dosari kubwa.

 Katibu wa CCM alipoulizwa kuhusu tuhuma hizi alisema kuwa ameiona barua iliyoandikwa na wanachama lakini alisema kuwa hawezi kuifanyia kazi maana haikuwa na orodha ya wanachama hao akashauri kuwa iwapo walioandika barua hiyo wapo basi waorodheshe majina yao wayawasilishe kwake ili tuhuma hizo ziweze kufanyiwa kazi, na alipoulizwa kuhusu tuhuma kwa mmoja wa wagombea kubainika kufanya hila ikiwemo rushwa alisema kuwa zipo kanuni zinazoongoza na hatua huchukuliwa kwa mtu wa aina hiyo ikiwemo kufutiwa matokeo na nyingine nyingi, akifafanua kuhusu mabasi ya mbunge kuwabeba wajumbe Katibu huyo alisema kuwa zipo njia zinazofahamika kwa mtu kuruhusiwa kubeba wajumbe ambapo ni kutumia simu na barua itakayokuwa imeandikwa na jumuiya hizo kuomba afanye hivyo na kama hakukuwepo na barua hilo ni kosa na hatua zitachukuliwa itakapothibitika kuwa kuna ukiukwaji wa kanuni za chama katika suala hilo.
Baada ya kuonyeshwa kwa ushirikiano huo na Taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mbunge aliacha kuingilia uchaguzi na baada ya hapo hakuonekana kabisa eneo la uchaguzi jambo lilipelekea uchaguzi wa UWT kufanyika kwa amani ambapo Jumuiya hiyo ilimpata mwenyekiti wake kwa njia zinazofaa.

 Wanachama wa CCM waliwamwagia sifa viongozi wa Mkoa waliokuwa wamekuja kusimamia zoezi la uchaguzi jinsi walivyokuwa wamesimama kidete kwa kutoonyesha kumtaka mtu kwa maslahi jambo ambalo wameomba viongozi mbalimbali Mkoani Shinyanga kuiga mfano wa viongozi hao safu iliyokuwa ikiongozwa na Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Shinyanga.
Wakizungumzia mchakato wa uchaguzi huo, Maafisa uchunguzi wa TAKUKURU Wilayani Kishapu wamesema kuwa bila msaada wa wan anchi wasingeweza kubaini kushamiri kwa vitendo vya rushwa pamoja na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wao mara wanapokuwa wana taarifa za Rushwa ili taasisi hiyo iweze kuzitokomeza.
Afisa wa TAKUKURU Bwana  Mlamuzi P Kuhanda amesema imefika wakati wananchi waiamini Taasisi hiyo na kwamba mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya UWT ni SALAMU tosha kwa wapenzi na wala Rushwa kuwa chaguzi zijazo wataongeza nguvu ya ziada kuhakikisha hawambakishi mtu hata kama angekuwa na cheo cha aina gani kwani walichotumwa ni kuhakikisha hakuna mtu anayeokoka baada ya kushiriki vitendo vya Rushwa.
Naye  Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Kishapu Bathromew Semhunge amesema kuwa alisikia mtu akijigamba kuwa Mwenye ndege hawezi kukwamishwa na Mto  ambapo nay eye akajibu kejeli hiyo kuwa mwenye ndege huyo amekwamishwa na kijito badala ya mto hii inathibitishwa na jinsi walivyoidhibiti mipango inayodaiwa kuratibiwa kwa umahiri mkubwa na mbunge wa jimbo la Kishapu na kupata mafanikio ya kumfanya akose usingizi na kushindwa kuonekana eneo la uchaguzi.
Mwandishi alipojaribu kumtafuta mbunge huyo kuzungumzia  tuhuma hizo simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.
Baadhi ya wajumbe walipohojiwa juu ya uchaguzi huu ulikuwa wa namna gani waliitupia lawama TAKUKURU kwa kudhibiti Rushwa jambo lilliowafanya washindwe kupata fedha na hivyo kuthibitika juu ya utendaji mzuri wa Taasisi hiyo, haikuishia hapo tu baada ya hapo zilikuja lawama kubwa dhidi ya mbunge toka kwa makundi ya wajumbe kwa kutelekezwa na mabasi yaliyokuwa yakiwasomba kuwaleta na baada ya kushindwa kwa kambi ya mbunge kwa mtu aliyemtaka wajumbe hao hawakula ambapo waliandamana hadi ofisi za chama cha Mapinduzi Wilaya kupata msaada jambo ambalo lilionyesha wazi pia juhudi za TAKUKURU.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.