Ads Top

UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA WANYAMA MKOANI KAGERA

Hapa ndipo yalipokuwa makazi ya Mzee Numbu Yihorogo na sasa anaishi kwa wasamalia wema
Hili ni zizi la Mzee Numbu Yihorogo likiwa halina kitu kwa sasa kufuatia ukiukwaji wa Haki za Binadamu
Mzee Numbu Yihorogo akiwa amebaki peke yake baada ya familia yake kutoweka na sasa hawajulikani walipo


Na Antony Sollo  Kashalunga
Hali iliyopo katika maeneo mbalimbali Mkoani Kagera inatisha na inatia huzuni kuona Watu sasa tunaelekea kuanza kubaguana kwa Makabila kinyume na Misingi  iliyowekwa na waasisi wa Taifa letu akiwemo haiyati  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mimi nimepewa taarifa za matukio haya ya unyama wa kutisha na hatimaye kwenda kuwaona viongozi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu na kufanya mazungumzo yaliyopelekea mimi kuanza safari ya kwenda Mkoani Kagera hususani Wilaya ya Muleba na Biharamuro ili kujionea hali ilivyo na ili niweze kutoa taarifa za kuaminika katika kituo chetu cha Sheria na Haki za Binadamu kuhusu maswahibu yanayowakumba wananchi hasa wa Kabila la wasukuma na baadhi ya makabila machache wanaoishi jirani na Hifadhi mbalimbali Mkoani humo.
Ndugu zangu,niliyoyaona na ambayo sasa si ya kusimuliwa,ni kweli nchi yetu inaelekea pabaya kwani tunaelekea kuanza kubaguana kwa Kabila zetu jambo ambalo ni hatari kuliko wakati wowote ule katika historia ya Uhuru wan chi yetu.
Huku kuna migogoro mikubwa inayopelekea shughuli za kijamii zikwame na pia wapo watu sasa wanaishi kama wakimbizi katika nchi hii ambayo katika medani za kimataifa  inasifika kwa kuwa nchi ya Amani na utulivu jambo ambalo si kweli, kuna familia zinazopata kufikia idadi ya kaya 1200 wakiwa wamechomewa nyumba zao,na si hivyo tu,kuna ngombe wanaokadiriwa kufikia 1600  waliopigwa risasi na maafisa wa wanyama pori Mkoani Kagera jambo ambalo ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu pamoja na wanyama.
 Kilichonisikitisha kuliko yote ni Kupotea kwa wanafamilia ya Mzee Numbu yihorogo ambapo hadi sasa amebaki maskini wa kutupwa na anaomba msaada wa Wanasheria kutoka kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ili asaidiwe kutoa sauti yake ili serikali iweze kuwajibishwa kufuatia watumishi wake kufanya unyama kwa raia na mali zao.
Ndugu zangu kuna matatizo makubwa huku kuna watu wamefuguliwa kesi za kubambikizwa baada ya kukaidi kutoa rushwa, wapo kina mama na watoto nimeshuhudia wakilala nje na kunyeshewa mvua na hawana chakula huku waume zao wakijaribu kutoroka kwenda kuangalia mahala pa kuishi ili kama watafanikiwa waweze kuwarudia ,wapo kina baba niliokutana nao jana wakitembea kwa miguu wakiondoka maeneo ya makazi walipokuwa wakiishi na kuelekea huku na kule mithili ya wakimbizi katika nchi yao,na leo wamenipigia simu kuwa tayari wamefika Chato tena wakitembea kwa miguu, naomba jamani Uongozi wa Juu wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu utafute namna ya kufika huku na kuweza kutoa msaada wa kisheria kwa kuwapeleka mahakamani watendaji wa serikali walioshiriki zoezi hili la ukatili kwa raia wan chi hii.
Haya ninayoyasema ninao ushahidi nimechukua mkanda wa Video sehemu mbalimbali za Mkoa huu ambapo nimuombe Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Mama Kijjo atoe tamko kali maana Bila hivyo huku hakufai wanyarwanda wamewanunua viongozi,wananchi hawasikilizwi kwa lolote na ninavyoona tutashuhudia maiti nyingi za raia hasa kina mama na watoto maana wanaachwa na waume zao na wengine hawana hata chakula na si kwamba wanaachwa kwa makusudi wakina baba wengine wamewekwa mahabusu na wana kesi mahakamani hata dhamana hairuhusiwi .
Kwa kweli huu ni ukatili wa kutisha  Shime wanaharakati wenzangu nawaomba tuungane tuweze kuwaokoa watu hawa maana hali ni Mbaya kibaya zaidi hata mawasiliano ni shida sana hasa katika maeneo ya tukio

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.