Ads Top

HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO TINDE MKOANI SHINYANGA AFANYA UKATILI KWA MAMA NA MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MITATU.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Tinde Mkoani Shinyanga leo tarehe 30/11/2012 amefanya ukatili kwa familia ya John Makomba kwa kuamua kutumia vibaya Mamlaka aliyopewa na kuutumikia Mhimili huo muhimu baada ya Wakazi wa kijiji cha Tinde kugombana na hatimaye kushitakiana katika mahakama hiyo.
 
Akizungumzia suala hili mtoa taarifa hizi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kupitia taarifa hii amesema, wanafamilia hao walipatwa na maswahibu hayo baada ya kutokea ugomvi kati ya mke wa John Makomba na Binti mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Anna ambapo imeelezwa kuwa walikuwa wamechelewa kufika Mahakamani hapo jambo ambalo lilipelekea Hakimu Denis wa Mahakama ya Mwanzo Tinde kuwaweka ndani wanandoa hao lakini ikwa ni ukiukwaji wa Sheria.
Majirani wa wanandoa hao wamesema kuwa wameshtushwa na kilio kilichokuwa kimeiandama nyumba ya Bwana na John Makomba na walipotaka kujua kulikoni waliambiwa kuwa mama wa mtoto huyo pamoja na mmewe walikuwa wamewekwa Mahabusu katika Mahakama ya Mwanzo Tinde kwa kosa la kuchelewa kufika mahakamani.
Habari zilizotolewa na ndugu wa karibu wa John Makomba zinadai kuwa kuchelewa kufika mahakamani kwa wanandoa hao kulitokana na kushindwa kupata  fedha mapema shilingi 100,000/= ambazo waliombwa kama Rushwa ili kupata dhamana  na Mh Denis ambapo baada ya kuzipata walianza safari ambapo walipofika tu waliamuriwa kuwekwa Mahabusu kwa kosa la kudharau Mahakama.
Nilipomtafuta Mh Denis kuzungumzia suala hili hakupatikana namba yake ilikuwa imezimwa na alikuwa Mjini Shinyanga kwa shughuli za Kikazi.
Kinachozidi kuikoroga akili yangu mpaka sasa ni juu ya kuwekwa Mahabusu familia yote wakati waliokuwa na ugomvi ni wanawake kwa wanawake lakini pia bila kujali Haki ya Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu najiuliza Mh Denis sijui ameupata wapi ujasiri wa kuitumia vibaya sheria namba 96 kuwakandamiza wanafamilia hawa.
Nilipowasiliana na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tinde alikiri kupokea nyaraka zilizokuwa zimeidhinishwa na Hakimu huyo ili kuwapeleka Gerezani wanafamilia hao pamoja na watu wengine na baada ya mazungumzo alisema kuwa suala hili liko kwenye Mhimili ambao nao una mamlaka kamili yanayotambuliwa na asingeweza kuingilia maamuzi ya Mhimili huo kwani kila Mhimili unajitegemea kwa mujibu wa sheria.
Ninachohitaji kutoka kwenu ndugu zangu ni kujua kuwa Iwapo Hakimu wa Aina hii ataamua kuitumia vibaya Ofisi yake maamuzi yake hayakubaliki kupingwa? binafsi naona Haki za Binadamu kwa wanandoa hawa zimekiukwa na si hivyo tu,Haki ya mtoto wa miaka mitatu wa wanandoa hawa pia imekiukwa maana amelala bila kula kwa siku ya leo ina maana Hakimu hana utu kiasi gani!!!!!
Nauomba uongozi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ulifuatilie kwa karibu suala hili kwani Mhakama ni mahali patakatifu na ndipo kwenye chimbuko la Haki ya aina yoyote,kama tunakuwa na Hakimu wa namna hii Haki itapatikana wapi!!!!!! sikubaliani na vitendo vilivyofanywa na Hakimu huyu kwa vile vimetokana na matakwa ya kujipatia fedha kwa njia ya Rushwa.
 
Taarifa hii imeandikwa na:
Antony Johnson Sollo
Mkurugenzi wa Shinyanga NguvuKazi Development Foundation SNDF
Kutoka Tinde Mkoani Shinyanga
+255 787 565 533/+255 713 565 533/+255 763 209 400

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.