Afrika Kusini imefufua matumaini yake ya kufuzu kwa raundi ijayo ya michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini
kwa magoli mawili
kwa bila, katika mechi yaon ya pili siku ya Jumatano.
Vijana hao wa Bafana Bafana walianza mechi hiyo vyema kuliko walivyocheza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Cape Verde.
Katika kipindi cha kwanza ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Angola.
Kunako dakika ya kumi na tano Afrika nusura
ifunge bao lakini msaidizi wa refa wa mechi hiyo aliinua kijibendera
kuashiria kuwa alikuwa ameotea.
Dakika mbili baadaye Bafana Bafana ilifanya shambulio lingine na mkwaju wa Siyabonga Sangwen ulikosa gola kwa ncha.
Kunako dakika ya 30 Siyabonga Sangweni akaifungia Afrika Kusini bao lake la kwanza.
Bao hilo lilionekana uwapa nguvu wachezaji wa Afrika Kusini ambao waliendeleza mashambulio yao dhidi ya Angola.
Malalamiko ya kocha
Afrika Kusini ingelifunga magoli zaidi katika
kipindi hicho lakini wachezaji wake kadhaa walikosa umakini wakati wa
kumalizia kwa kupoteza pasi nzuri walizopewa na wakati mwingine kupiga
mpira ovyo.
Hata hivyo juhudi zao hazikufanikiwa na kufikia wakati wa mapunziko Afrika Kusini ilikuwa ikiongoza kwa bao moja kwa bila.
Kabla ya mechi hiyo kocha wa Afrika Kusini
alikuwa amewashutumu wachezaji wake kwa kukosi umakini wakati wa mechi
muhimu na inaonekana kuwa mazungumzo yake na wachezaji wake imeonekana
kuzaa matunda.
Kipindi cha pili kilianza huku Angola ikiwa na
wachezaji kumi pekee baada ya refa wa mechi hiyo kuanza mpira kabla ya
kuruhusu mabadiliko katika kikosi cha Angola.
Kinyume na iliyokuwa katika kipindi cha kwanza
wachezaji wa Angola walianza kuonana na kufanya mashambulio kadhaa
katika lango la Afrika Kusini.
Lakini, licha ya juhudi hizo, Afrika Kusini
ilipata bao lake la pili kunako dakika ya 61 kupitia kwa mchezaji wake
wa ziada Lehlohonolo Majoro, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika
mbili tu kabla ya kufunga bao hilo.
Mshambulizi matata wa Angola, Manucho ambaye
alitarjiwa kukiongoza kikosi chake kushinda mechi hiyo, alithibitiwa na
zaidi ya wachezaji wawili wa Afrika Kusini, mara tu alipopewa pasi.
Angola sasa ni sharti ishinde mechi yake ya
mwisho dhidi ya Cape Verde siku ya Jumapili na iombe Morocco itoke sare
na Cape Verde katika mechi yao ya Jumatano ili iweze kufuzu kwa hatua ya
robo fainali.
Hata hivyo huenda maombi hayo yasitimie ikiwa
kutakuwa na mshindi wa mechi ya leo na hivyo Angola italazimika kusubiri
matokeo ya mechi kati ya Afrika Kusini na Morocco siku ya Jumapili ili
kufahamu ikiwa imeyaaga mashindano hayo au la
No comments: