Ads Top

Morocco yatoka sare na Cape Verde


Wachezaji wa Cape Verde kabla ya mechi hiyo

Cape Verde imeandikisha historia kwa kufunga bao lake la kwanza katika fainali za mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
Cape Verde, amabyo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza imetoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na mabingwa zamani wa kombe hilo Morocco, katika mechi ya nne ya kundi A.
Cape Verde, ilipata bao lake kunako dakika ya 36 kupitia kwa nyota wake Platini, ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa mshambulizi Ryan Mendes
Morocco, ilianza mechi hiyo ikiwa na matumaini makubwa ya kuimarisha nafasi yake ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo, kwa kunadikisha ushindi wao kwa kwanza.
Nyota wa Morocco, Younes Belhanda, wa klabu ya Montepilier ni miongoni mwa wachezea wa Tunisia katika mechi hiyo.
Belhanda alijumuishwa katika kikosi hicho ili kuimarisha safu ya mashambulizi baadaya wa Morocco kutoka sare mechi yake ya ufunguzi.

Cape Verde yapania kushinda mechi yake ya kwanza


Younes Belhanda

Ila tangu kipenga cha mwanzo, Cape Verde ilionekana kuilemea miamba hao wa Afrika Kaskazini.
Kocha wa Cape verde Luis Antunes, ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake ambacho kinashiriki katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza watashinda mechi hiyo.
Juhudi za Morocco kusawazisha katika kipindi cha kwanza hazikufua dafu.
Dakika za kwanza arubaini na tano zimekamilika na Cape Verde iko kifua mbele kwa bao moja kwa bila.
Lakini kunako dakika ya sabini na nane Morocco ilizawazisha na kufanya mambo kuwa moja kwa moja.
Cape Verde, sawa na Morocco, ilitoka sare ya kutofungana bao lolote katika mechi yao ya ufunguzi, lakini ilionyesha mchezo mzuri kuliko wapinzani wao Afrika Kusini.
Afrika Kusini inaongoza kundi hilo la alama nne na inahitaji kutoka sare mechi yake ya mwisho ya makundi ili kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
Cape Verde na Morocco zinashikilia nafasi ya pili na alama mbili kila mmoja huku Angolo ikivuta mkia.
Timu hizo tatu sasa ni sharti zishinde mechi zao za mwisho ili kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
Siku ya Alhamisi Mali inacheza na Ghana kisha Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoa udhia Niger 
]katika mechi za kundi B


Kikosi cha Morocco  Kikosi cha Cape Verde
01 Lamyaghri
02 Chakir
03 Bergdich
05 Benatia
17 El Adoua
07 Barrada
08 El Ahmadi
10 Belhanda
11 Assaidi
14 El Hamdaoui
21 Amrabat
Wachezaji wa ziada            
01 Lamyaghri
02 Chakir
03 Bergdich
05 Benatia
17 El Adoua
07 Barrada
08 El Ahmadi
10 Belhanda
11 Assaidi
14 El Hamdaoui
21 Amrabat
01 Vozinha
03 Varela
06 Neves
08 Varela
14 Gege
18 Nivaldo
05 Babanco
07 Platini
15 Soares
11 Tavares
20 Ryan

Wachezaji wa Ziada
12 Fock
16 Rilly
13 Lima
19 Pecks
23 Carlitos
02 Stenio
04 Ramos
17 Souto
22 Silva
09 Rambe
10 Heldon
21 Djaniny

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.