Ads Top

CHAMELEONE HUENDA AKAFUNGULIWA KESI YA MAUAJI

 
Joseph Mayanja aka Chameleone na mkewe Daniella Atim.
POLISI nchini Uganda wanaendesha uchunguzi ambao huenda wakamfungulia mashitaka ya mauaji mwanamuziki ‘chakaramu’, Joseph Mayanja aka Chameleone, mkewe Daniella Atim na kundi la muziki la Leon Island.
 
Marehemu Robert Karamagi akiwa katika Hospitali ya Mulago baada ya kukumbwa na majeraha nyumbani kwa Chameleone.
Hii ni kutokana na kifo cha Robert Karamagi, 27, aliyefariki katika Hospitali ya Mulago baada ya kukumbwa na majeraha aliyoyapata nyumbani  kwa mwanamuziki huyo huko Seguku.
Akihojiwa na gazeti la Sunday Vision, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kajjansi, Ibrahim Saiga, alisema wamechukua ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani na mashuhuda walioona, ushahidi ambao unapingana na ule uliotolewa na familia ya Mayanja.
Pamoja na kusema kwamba faili la uchunguzi huo litapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kwa ushauri,  Saiga alisema baba wa Karamagi alikana kwamba mwanaye alijimwagia mafuta na kujiwasha moto.
Pia alisema kwamba mwanaye huyo alimwita kwenda hospitalini hapo ambapo alimwambia alikuwa ameteswa, akafungwa kamba, akamwagiwa mafuta na kuchomwa moto na mwanamuziki huyo na wenzake wa kundi lake.
Alhamisi iliyopita, Chameleone alihojiwa na wapelelezi kwa muda mrefu, lakini aliachiwa kwa dhamana.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.