WANANCHI MLANDIZI WALALAMIKIA UTENDAJI WA JESHI LAPOLISI
Bwana Ally akionyesha kidole chake kilichokatwa na mapanga walipovamiwa katika tukio hilo
majeraha mkono wake wa kushoto ambapo umepinda baada ya kushambuliwa na majambazi
Mguu wa mjukuu wa mwenyekiti huyo Nusura Karim uliokatwa panga katika tukio hilo
Mme wa M.kiti huyo Bwana Ally Ngwallu akiwa na majeraha kichwani baada ya kukatwa katwa kwa mapanga katika tukio hilo
Mtoto huyo akiwa na Babu yake
Mwenyekiti akiwa na makovu baada ya kukatwa mapanga mapanga
Watishia kuwashtaki watendaji wa Jeshi hilo kwa IGP
Kesi zikifunguliwa watuhumiwa huachiwa katika mazingira tata Ni pamoja na za Unyang’anyi wa kutumia silaha
Na Antony Sollo Kibaha
Jeshi
la Polisi kituo cha Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani limeendelea
na kigugugmizi katika masuala mbalimbali ikiwemo kushindwa kusimamia
majukumu ya kuanzishwa kwa jeshi hilo yaani kulinda raia na mali zao
Akiongea
kwa huzuni kubwa mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Abdalla
mkazi wa kitongoji cha Msongola kata ya Janga amesema tumesikitishwa
sana na utendaji wa jeshi la polisi kwa kushindwa kusimamia majukumu
yake hususani kulinda raia na mali zao,hii inatokana na matukio
mbalimbali yaliyotokea miezi michache iliyopita lakini pamoja na Jeshi
hilo kupatiwa taarifa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi leo.
Matukio hayo ni pamoja na kuvamiwa kukatwakatwa kwa mapanga Mwenyekiti wa Kitongoji chetu Nusura Ngwallu
pamoja na familia yake tukio ambalo liliripotiwa kituoni hapo lakini
hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa na jeshi hilo tukio ambalo
limepelekea kujeruhiwa vibaya kwa wanafamilia hao na watu watuhumiwa
walipokamatwa mara ya kwanza walihojiwa na kukiri kuwa walitumwa na mtu
ambaye anadaiwa kuwa ana mgogoro wa maeneo na wananchi wa kitongoji
hicho huku mwenyekiti wa kitongoji hicho akisimamia Haki za raia ambazo
zilitaka kuporwa na mwekezaji huyo lakini maajabu hadi leo
hawajafunguliwa kesi yoyote na jeshi hilo.
Zipo
tuhuma mbalimbali zinazomlenga moja kwa moja Mkuu wa kituo cha Polisi
Mlandizi kwa kutuhumiwa kutumiwa na wafanyabiashara mbalimbali na
wawekezaji kwa lengo la
kuwakumbatia katika matukio mbalimbali hii ni pamoja na kujiingiza katika migogoro ya
Ardhi katika maeneo hayo ambapo kuna kesi mbalimbali ambazo
hazifunguliwa mpaka sasa huku taarifa zikidai kuwa watuhumiwa wa kesi
hizo wamekamatwa na kuachiwa hivyo kutofikishwa mahakamani.
Mwandishi
wa Habari alimtafuta Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msongola ili kujua
ukweli wa tuhuma zinazolikabili Jeshi la Polisi Wilayani Kibaha ambapo
alikuwa na haya.
Ndugu mwandishi mimi kwa jina naitwa Nusura Ngwallu ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msongola Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani tukio la
kuvamiwa na kukatwa katwa na mapanga lilitokea jumatatu tarehe
02/10/2012 majira ya saa 7 usiku hapa nyumbani kwangu na ripoti katika
kituo cha polisi Mlandizi na watu waliofanya tukio hilo baadhi yao
tuliwatambua na hadi sasa waliachiwa tu na wanaendelea kutamba mtaani
jambo linalotuondolea imani na jeshi la polisi maana kigugumizi cha
kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani kinaonyesha wazi udhaifu
mkubwa katika utendaji wa Jeshi hili.
Ndugu
mwandishi inashangaza kuitwa mahakamani na kukuta washtakiwa
hawajafunguliwa kesi yoyote najiuliza hivi kweli watendaji wa jeshi la
polisi katika kituo cha polisi Mlandizi wanajua vizuri wajibu wao au
wamejaa ubabaishaji na maslahi binafsi!
Inasikitisha
sana juzi nimeletewa ujumbe kuna mtu anadai kuwa iwapo nitaendelea
kusimamia msimamo wangu katika mgogogro wa Ardhi kati ya wananchi na
Mwekezaji safari hii nitauawa maana kuvamiwa kwangu kumbe sijajifunza
kitu.
Nimeshangazwa
na kuanza kuandamwa mpaka na viongozi wa Chama changu kwamba siwajibiki
huku wakijua kuwa ninaumwa na taarifa ya Daktari ipo na ameshauri
nipumzike mpaka nitakapopona ili niendelee na majukumu yangu ambapo sasa
inaonekana baadhi yao
wanatumiwa ili kuniondoa katika nafasi hii ili wafanikishe uporaji wa Ardhi ya wananchi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msongola Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Nusura Ngwallu umri wa miaka 43 hadi sasa anatishiwa kuuawa na watu wanaodaiwa kuwa wametumwa na mwekezaji aliyepora maeneo ya wananchi wa kitongoji cha Msongola Wilaya ya
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msongola Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Nusura Ngwallu umri wa miaka 43 hadi sasa anatishiwa kuuawa na watu wanaodaiwa kuwa wametumwa na mwekezaji aliyepora maeneo ya wananchi wa kitongoji cha Msongola Wilaya ya
Kibaha Mkoani Pwani ambapo tukio hili la kuvamiwa na kukatwa na mapanga yeye na mme wake pamoja na mjukuu wao Nusura Karim umri wa miaka 2
lilitokea jumatatu tarehe 02/10/2012 majira ya saa 7 usiku huko
nyumbani kwake na ripotiwa katika kituo cha polisi Mlandizi lakini
hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa watu wanaotuhumiwa kumvamia
mwenyekiti huyo kwa lengo la kumuua yeye na mme wake Bwana Ally Ngwallu
mwenye umri wa miaka 53 wote wakazi wa Kitongoji cha Msongola.
Mkuu
wa Kituo hicho alipotafutwa kujibu tuhuma zinazotolewa na wananchi hao
akiwemo mwenyekiti wa Kitongoji hicho simu yake ilikuwa ikitumika muda wote ambapo juhudi za kumtafuta zinaendelea
Tanzanian Shilling Converter
No comments: