Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akagua miradi ya maendeleo ikiwemo soko la kimataifa la pamoja na ujenzi wa daraja mpakani mwa tanzania na burundi, kibondo mkoani kigoma
Jengo la Soko la Pamoja lililokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema jana jioni,ikiwa
na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine
kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua Soko la Pamoja jana jioni. 

Katibu
Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Mpya ya
Kokonko Bwa.Peter Toima (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango (shoto) na baadhi ya Wanachi
wakielekea kukagua Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi
wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya
mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini
vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya
Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano na
Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo
unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji
na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya
Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
Pichani
ni Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha
Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya
kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya
Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya
Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano
na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart
Fund.
Mradi
huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya
Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na
Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
Mradi
huo unaotarajiwa kukamilika februari 20,2013 utagharimu kiasi cha
shilingi 260,000,000/=,aidha imeelezwa kuwa mradi huo utatekelezwa kwa
awamu nne,awamu ya kwanza imeshaanza ambayo unahusisha ujenzi wa
daraja,barabara KM1 inayotoka kwenye soko hadi darajani na hifadhi ya
Mazingira,utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia 70% mpaka sasa.

Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi
wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye
mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na
bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha
nchini Burundi.
Msimamizi
wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai akitoa
ufafanuzi mbele ya Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana kuhusiana na
ujenzi wa Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha
Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya
kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya
Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya
Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano
na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart
Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia
ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya
Nyabibuye.
Katibu
Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya
Nyamtukuza iliopo kwenye Wilaya ya Kibondo,mkoani Kigoma,pichani shoto
ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi.
Katibu
Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya
Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango wakikagua ujenzi wa shule hiyo ya Nyamtukuza
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kushoto akishiriki kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyamtukuza
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyamtukuza mara baada ya kuwahutubia mapema jana mchana,kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyamtukuza mapema jioni ya jana,Kinana
aliuahidi uongozi wa shule hiyo kuwapa umeme (Solar Pannel )mbili kwa
ajili ya kuzalisha umeme shuleni hapo,Kampyuta moja pamoja na Televishen
Katibu
Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi wa kijiji cha
Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutanno wa hadhara mapema jana jioni na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Sehemu
ya shamba la Mahindi safi kabisa,ambalo pia Ndugu Kinana aliwahimiza
wanakijiji cha Rumashi,kutumia Pembejeo za mbolea kuhakikisha wanapata
mazao bora.
Katibu
Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha
Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko mapema jana jioni.
No comments: