Ligi kuu ya Vodacom tanzania bara imeaza kwa mzunguuko wa pili huku timu za Simba, Azam zaanza kwa kishindo
MABINGWA watetezi, Simba jana walianza kwa kishindo duru la pili Ligi Kuu Bara kwa kuitungua African Lyon mabao 3-1, katika mechi ambayo kila upande ulikosa kufunga penalti katika kila kipindi.
Ushindi kama huo pia uliandikwa na Azam FC
iliyotumia vizuri Uwanja wa Chamazi kuiogesha kipigo Kagera Sugar ya
Kagera, kadhalika Coastal Union kule Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo
Shooting.
Simba imefikisha pointi 26, lakini ikiendelea
kubaki nyuma ya Azam kwa tofauti ya pointi moja, na Yanga inayocheza leo
haijaathiriwa na matokeo ya mechi za jana.
Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wachezaji Mrisho Ngassa wa Simba na
Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wachezaji Mrisho Ngassa wa Simba na
Shamte Ally wa Lyon walikosa penalti. Penalti ya
Ngassa ingeweza kumpa ‘hat trick’ kama siyo kipa wa Lyon, Abdu Seif
kuicheza dakika ya 66 kufuatia Ibrahim Issac kumkwatua Ramadhan
‘Redondo’ Chombo.
Shamte naye alishindwa kulenga lango baada ya
penalti yake kwenda nje kufuatia madhambi ya Paul Ngalema dhidi ya Fred
Lewis dakika ya 30.
Redondo alifunga bao la mapema zaidi mzunguko wa
pili, baada ya kutumia dakika mbili tangu kuanza mpira kutikisa kamba za
Lyon akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa.
Lyon walijibu shambulizi dakika ya nne na ustadi wa Juma Kaseja ulimnyima bao Jacob Massawe baada ya shuti lake kuchezwa na kipa huyo namba moja Msimbazi.
Lyon walijibu shambulizi dakika ya nne na ustadi wa Juma Kaseja ulimnyima bao Jacob Massawe baada ya shuti lake kuchezwa na kipa huyo namba moja Msimbazi.
Mashuti mawili ya Ngassa dakika ya 4 na 6
yangeweza kubadilisha matokeo kama siyo kukosa shabaha na kwenda moja
kwa moja mikononi mwa kipa wa Lyon, Abdul Seif.
Ngassa alirekebisha makosa yake kwa kufanya
matokeo kuwa 2-0 baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Lyon akimalizia pasi
ya Jonas Mkude.
Alikuwa Ngassa tena akipachika bao la tatu, la
pili kwake kwenye mchezo huo shuti akimalizia mpira wa krosi uliopigwa
na Haruna Chanongo dakika ya 35. Kipindi cha pili, Kocha Patrick Liewig
aliwapumzisha Paul Ngalema na Mussa Mudde na kuingia Kigi Makasi na
Komalibil Keita.
Lyon walipunguza makali ya tofauti ya mabao ya
kufungwa baada ya Bright Ike kumtungua Kaseja dakika ya 60 likiwa bao
pekee kwao kwenye mchezo huo.
Pamoja na ushindi huo, Kocha Liewig alisema mchezo
ulikuwa mgumu, ingawa pia hakusita kueleza hisia akiwalaumu wachezaji
wake kucheza ovyo kipindi cha pili.
Mkwakwani Tanga, Union walifikisha pointi 25 na
kupanda mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo kwa mabao ya Philipo
Mutasela, Danny Lihanga na Haroun Mahundi, huku bao la Mgambo likifungwa
na Peter Mwaliyanzi. Kwenye Uwanja wa Chamazi, Ncha Hamis alifunga mara mbili na Abdi Kassim akamalizia maumivu kwa kufunga bao la tatu.
No comments: