Mahujaji waogelea katika mto Ganges India
Mamilioni wanatarajiwa kuogelea kwenye mto huop mwishoni mwa leo
Mahujaji waoga mto Ganges
Maelfu ya watu wamekuwa wakioga katika makutano ya mito miwili ya Ganjes na Yauna eneo la Allahabad nchini India.
Ni katika siku ya kwanza ya tamasha la Kumbh Mela.
Takriban mahujaji milioni kumi wanatarajiwa kuogelea katika mtu huo hadi kufikia mwishoni mwa leo.
Tamasha hili ambalo hufanyika kila baada ya
miaka kumi na miwili, ni mojawapo ya mikusnayiko mikubwa ya watu
duniani. Zaidi ya watu milioni 100, wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo
litakalodumu miaka 55
Waumini wa dini ya Hindu wanaamini kuwa
wakiogelea katika mto huo , dhambi zao zitafutika na kisha itawasaidia
kupata msamaha na kuokoka kutokana na dhambi.
Mnamo mwaka 2001, zaidi ya watu milioni 40
walikusanyika katika siku rasmi ya kuogelea kwenye mto huo na kuvunja
rekodi ya idadi kubwa ya watu kuwahi kukusanyika katika sehemu moja
duniani.
Wahindi wanaamini kuwa asali ilianguka kwenye
mto huo kufuatia vita kati ya miungu na mashetani waliokuwa
wanaipigania, na baada ya hapo imekuwa desturi ya wahindi kuogelea
kwenye mto huo.
Waumini waliomba wakati wakioga katika makutano ya mito hiyo miwili ya Yamuna na Ganges kuanzia hapo jana.
Mji wa Allahabad umekuwa ukijiandaa kwa tamasha hilo kwa miezi mingi na watu wameweka mahema kuuzingira mto wenyewe.


Tanzanian Shilling Converter
No comments: