Matajiri waweza lisha mafakiri wote
Shirika la msaada la kimataifa, Oxfam, linasema kuwa watu 100 tajiri
kabisa duniani walipata fedha za kutosha mwaka jana za kuweza kumaliza
ufukara wa watu maskini kabisa duniani, mara nne zaidi.
Oxfam inasema kuwa mwaka jana pato la matajiri wakubwa kabisa 100 lilikuwa jumla ya dola 240 bilioni.
Na watu maskini kabisa wanatumia dola moja na robo tu kwa siku.
Katika taarifa iliyotoa kabla ya mkutano wa
kiuchumi wa Davos, Usiswi, juma lijalo, Oxfam imesema kuzidi kwa utajiri
mkubwa duniani unazuwia juhudi za kupambana na umaskini.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: