Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wanakutana nchini Ivory Coast kwa kikao maalumu kuhusu Mali.
Katika kikao chao cha faragha wametoa wito wa msaada zaidi wa kimataifa katika kile walichoita vita dhidi ya ugaidi.
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa,
Laurent Fabius, ambaye anahudhuria mkutano huo, ametoa wito wa wanajeshi
wa Afrika kutumwa Mali haraka na kuanza kutumika.
Akihutubia mkutano wa nchi za Afrika Magharibi,
Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, alisema
jambo muhimu ni kufanya haraka kutuma wanajeshi Mali.
Alithibitisha kuwa Ufaransa itaongoza ujumbe wa Ulaya mwezi ujao ili kusaidia kulifunza na kulijenga tena jeshi la Mali.
Bwana Fabius piya aliwasihi washirika wa kimataifa wa Afrika wasaidie kwa usafiri na fedha.
Alieleza kuwa mkutano wa wafadhili utafanywa
mjini Addis Ababa mwisho wa mwezi, na alisema mkutano huo utakuwa muhimu
kushughulikia mahitaji ya Mali na kanda hiyo.
Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast, ambaye
ndiye mwenyeji wa mkutano wa Abidjan, alisema wakati umefika kwa mataifa
na mashirika makuu kuonesha mshikamano zaidi na kujitolea kuisaidia
Afrika na Ufaransa.
No comments: