Wanajeshi wa Ufaransa, nchini Mali, wameweza kudhibiti uwanja wa ndege katika mji muhimu wa Timbuktu.
Kwa mujibu wa afisaa majeshi ya hayo, waliudhubiti mji huo bila upinzani kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.
Wanajeshi wa Mali na Ufaransa, wamekuwa wakipigana kuelezea Kaskazini mwa nchi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Siku ya Jumamosi , waliuteka mji wa Gao, mji wenye idadi kubwa ya watu nchini Mali.
Maelfu ya watu walikusanyika kwenye barabara za mji kusherehekea kuwasili kwa wanajeshi hao.
Wapiganaji wa kiisilamu waliteka eneo la
Kaskazini mwa nchi mwaka jana lakini wamekuwa wakishindwa tangu majeshi
ya Ufaransa kuanza kuwashambulia mapema mwezi huu.
Mwandishi wa BBC nchini Mali anasema Wafaransa wanatarajiwa kuikomboa Timbuktu bila ya tatizo. bofya hapa kwa habari zaidi..>>>>
No comments: