Katibu wa Bunge, Spika Makinda wapingana
Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah.
KATIBU wa Bunge, Thomas Kashilillah amepingana hadharani na bosi wake Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhusu kurushwa moja kwa moja matangazo ya Vipindi vya Bunge.
KATIBU wa Bunge, Thomas Kashilillah amepingana hadharani na bosi wake Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhusu kurushwa moja kwa moja matangazo ya Vipindi vya Bunge.
Jana katika mkutano na waandishi wa habari katika
Ofisi za Bunge, Kashilillah alisema kuwa ofisi yake inakusudia
kutoonyesha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge vinavyofanyika
mjini Dodoma kutokana na baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za kibunge
kwa kuvunja maadili.
Hata hivyo, kauli ya Kashilillah inapingana na ile
ya Makinda aliyoitoa mjini Dodoma, Februari 8 wakati wa kuahirisha
kikao cha 10 cha Bunge aliposema: “Naipongeza TBC (Shirika la Utangazaji
la Taifa) kwa kuonyesha moja kwa moja matangazo na yote yanayoendelea
bungeni.
“Kutokana na vurugu zilizotokea, ninaiomba
Serikali kuiongezea ruzuku TBC ili kupata mitambo ya kisasa waweze
kuonyesha vizuri matangazo yake, safari hii matangazo yalikuwa
yanakatika katika sana,” alisema Makinda.
Hata hivyo, kauli hiyo wakati wa kufunga Bunge
ilikuwa ni ya pili kwa Makinda kwani baada ya kutokea vurugu
zilizoongozwa na baadhi ya viongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,
Makinda aliisifu TBC kwa kuonyesha kila kilichotokea bungeni na kuweka
msisitizo kuwa lazima TBC isaidiwe ili kila kinachotokea ndani ya Bunge
kionekane kwa wananchi.
Akizungumza jana kwenye Ofisi za Bunge,
Kashilillah alisema kuwa vikao vinavyofanyika sasa mara nyingi vinakiuka
kanuni na maadili ya shughuli za Bunge, jambo ambalo limesababisha
baadhi ya wabunge kuinuka na kutoa kauli mbalimbali wakati mijadala
ikiendelea.
Kashilillah alisema, utaratibu unafanyika na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kuangalia namna ambavyo
wataweza kuonyesha shughuli za Bunge kwa vipande vipande vilivyorekodiwa
kwa maeneo yanayofuata kanuni na maadili ili kuficha taswira mbaya
itakayojitokeza kwa wananchi.
“Kuna ukiukwaji mkubwa wa kanuni na maadili ya
vikao vya Bunge, na si kwamba wanaofanya hivyo hawafahamu, isipokuwa
wanafanya makusudi au wanatafuta umaarufu kupitia vikao hivyo. Kutokana
na hali hiyo, tumeamua kukaa na TCRA ili kuangalia namna ambavyo
tunaweza kurusha vikao vilivyorekodiwa badala ya moja kwa moja,”
alisema.
Simu za matusi na kashfa
Akizungumzia suala la Spika Makinda kutukanwa na kukashifiwa, Dk Kashililah alisema kuwa, kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali ameshawafahamu wote waliofanya hivyo na taratibu za kuwakamata zinaandaliwa.

“Tumeshawabaini, tunafahamu wanakoishi na namba
zao tayari zimeanza kushughulikiwa. Hasa wale wote waliotuma ujumbe wa
matusi au kupiga simu,” alisema.
Kuvunjwa kwa kamati
Kuhusu kuvunjwa kwa baadhi ya Kamati za Bunge, alisema kuwa Spika wa Bunge anaweza kuzivunja kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo utendaji wake au ushauri unaotoka kwa viongozi wa vyama vyenye uwakilishi bungeni.

Alisema kutokana na hali hiyo, waliangalia kamati
ambazo zinafanya kazi kwa mwingiliano na kuhamishia shughuli zile kwenye
kamati nyingine kama ilivyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma
(POAC) ambayo shughuli zake zimehamishiwa kwenye Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC).
kwa habari zaidi bofya hapa..>>>
kwa habari zaidi bofya hapa..>>>
No comments: