ARSENAL WAIBUKA NA USHINDI
Olivier Giroud afunga bao
Arsenal wafunga 2-0 lakini watolewa
Licha ya kuifunga Bayern Munich ya Ujerumani mabao
mawili kwa bila ugenini, Arsenal waondolewa katika mashindano ya Klabu
bingwa bara Ulaya.
Hii ni kwa sababu katika mechi ya awali
iliyochezwa wiki mbili zilizopita katika Uwanja wa Emirates, Arsenal
walifungwa magoli 3-1 na Bayern.
Mchezaji Olivier Giroud aliipatia
'The Gunners' goli lao la kwanza katika dakika ya 15 baada ya pasi safi
kutoka kwa Theo Walcott.
Kufuatia bao hilo Arsenal wakawa wanahitaji magolo mengine mawili ili kumaliza mechi wakuwa juu kwa 3-0.
Mlinda lango wa Arsenal Lukasz Fabianski
alifanya kazi ya ziada kwani alipangua mikwaju kadhaa kutoka kwa
mshambulizi matata Arjen Robben hivyo kumnyima nafasi ya kuifungia
Bayern Munich goli lolote.
Lakini baada ya mechi , Bayern Munich ndio walifaulu kuingia hatua ya robo fainali.
No comments: