Waziri wa afya wa Afrika Kusini: Amesema kuwa zaidi ya asili mia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi

wasichana wengi waathirwa na HIV nchini Afrika Kusini
Waziri wa afya wa Afrika Kusini
Amesema kuwa zaidi ya asili mia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa
virusi vya Ukimwi, ikilinganishwa na asili mia 4% tu ya vijana wa shule.
Hii ameelezea ni kutokana pakubwa na kuongezeka
kwa mababa sukari au kwa jina lingine, *fataki*, ( Wazee wanao tembea na
wasichana wadogo kwa umri).
Waziri
Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa wasichana wengi
wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala ya kuwa
na vijana wa rika lao.
Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asili
mia kumi ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo
imekuwa na mradi wa kuvuma zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya
virusi hivyo vya HIV , ARV tangu rais Jacob Zuma alipomteua bwana
Motsoaledi kuongoza wizara hiyo ya afya yapata miaka minee iliyopita. Kwa habari zaidi bofya hapa..>>>>
No comments: