CORD wadai hujuma kwenye uchaguzi Kenya
Mgombea mwenza wa waziri mkuu wa
Kenya Raila Odinga, amesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa kuna
hujuma dhidi yao katika dhughuli ya kuhesabu kura inayoendelea katika
ukumbi wa Bomas, na kwamba shughuli hiyo inastahili kusitishwa.
Hata hivyo alisema kuwa haina maana kuwa wanaitisha maandamano.
Shughuli ya kuhesabu kura ingali inaendelea
ingawa kwa mwendo wa kinyonga baada ya tume hiyo kutupilia mbali mitambo
yake ya kuhesabu kura baada ya kugoma.
Uhuru Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya
kura za wagombea wa urais akiwa na kura 2,660,379 dhidi ya mpinzani wake
Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini matokeo rasmi yatajulikana
tu mwishoni mwa juma.
Taharuki imetanda na kuna hali ya wasiwasi kwani
tume ya uchaguzi haijatangaza matokeo ya urais zaidi ya masaa arobaini
na nane tangu wakenya kupiga kura.
Muungano wa CORD umesema kuwa unatafakari hatua
za kuchukua baada ya kudai hujuma katika shughuli inayoendelea ya
kuhesabu kura za urais.
Shughuli hiyo imekumbwa na utata hasa baada ya mitambo ya kuhesabu kura ya tume ya uchaguzi kukumbwa na hitilafu.
Hatua hii imelazimu tume hiyo kuanza kuhesabu
kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais kwenye
ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa
Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari mjini Nairobi na kusema
kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu kura za urais
kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi kutoka kwa
makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa
Musyoka vile vile amesema kuwa muungano huo una
tashwishi kuhusu baadhi ya matokeo wakisema sio ya kweli kwa kuwa
hayawiani na yale waliyoyaleta maajenti wao.
Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa.
Musyoka amesisitiza kuwa tatizo hilo limetokana
na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura na pia kuanza upya kwa shughuli ya
kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani
kwa habari zaidi bofya hapa...>>>>
kwa habari zaidi bofya hapa...>>>>
No comments: