Afrika Kusini kuondoa wanajeshi 'CAR'
Afrika Kusini, inasema kuwa
itawaondoa wanajeshi wake kutoka Jamuhuri ya Afrika ya Kati, baada ya
waasi kupindua serikali zaidi ya wiki moja iliyopita.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa mkataba kati ya nchi hizo mbili umetupiliwa mbali baada ya kung'olewa kwa rais Francois Bozize.
Bwana Zuma anakabiliwa na hasira za wananchi baada ya wanajeshi 13 wa nchi hiyo kuuawa katika mapinduzi ya kijeshi .
Alitoa tamko hilo katika mkutano wa dharura
kuhusu mgogoro wa kisiasa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambao
marais wa nchi za magharibi walikataa kumtambua kiongozi wa waasi kama
rais wa taifa hilo.
Michel Djotodia alitangaza kuwa ataitawala nchi hiyo kwa kipindi cha mpito, baada ya kundi la waasi wa
Seleka kuvamia mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui, na kumaliza uongozi wa aliyekuwa rais Bozize, aliyetawala kwa mwongo mmoja.
Seleka kuvamia mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui, na kumaliza uongozi wa aliyekuwa rais Bozize, aliyetawala kwa mwongo mmoja.
Kiongozi huyo wa waasi amesema ataongoza nchi hiyo hadi uchaguzi utakapofanyika mwaka 2016.
''Haiwezekani kwetu kumtambua mtu aliyejitangaza kama rais,'' alisema rais wa Chad, Idriss Deby wakati wa mkutano huo.
Alisema Zuma aliwaambia viongozi hao kuwa anapanga kuondoa majeshi yake nchini humo.
Afrika Kusini ilikuwa na takriban wanajeshi, 200
mjini Bangui, ambao kazi yao ilikuwa kujaribu kuzuia waasi wa Seleka
kumng'oa mamlakani bwana Bozize ambaye kwa sasa yuko nchini Cameroon.
Pamoja na wanajeshi 13 kuuawa, wengine 27
walijeruhiwa, ikiwa idadi kubwa ya wanajeshi kuwahi kuuawa nje ya nchi
hiyo tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994.


Tanzanian Shilling Converter
No comments: