RAILA, KALONZO WAENDA IKULU KWA RAIS UHURU KENYATTA
RAILA KUSHOTO NA KALONZO KULIA
Nairobi. Vigogo wa
Muungano wa Demokrasia na Mageuzi (Cord) wa Kenya, Raila Odinga na
Kalonzo Musyoka wamerudi kutoka nchini Afrika Kusini na kumtembelea Rais
Uhuru Kenyatta.
Ujio huo wa Odinga kwa mujibu wa msemaji wake, Dennis Onyango lengo lilikuwa kufahamiana na kujadiliana masuala muhimu ya nchi.
Ujio huo wa Odinga kwa mujibu wa msemaji wake, Dennis Onyango lengo lilikuwa kufahamiana na kujadiliana masuala muhimu ya nchi.
Katika maongezi yao na Rais Kenyatta viongozi hao
wa Muungano wa Cord walisema kwamba watahudhuria sherehe za kufunguliwa
kwa Bunge la 11 nchini humo.
Akidhibitisha mbele ya waandishi wa habari taarifa
za kuhudhuria sherehe hizo za kufunguliwa kwa Bunge hilo kwa viongozi
hao Onyango alisema kwamba hayo ni makubaliano kati ya Uhuru na viongozi
hao.
Alisema viongozi hao pia walijadiliana kuhusu namna ya kukabili masuala yatakayowasilishwa bungeni kwa mtazamo wa kuridhiana.
Kwa sasa Muungano wa Jubilee unaounda serikali
unamiliki mabunge yote mawili, huku maspika Justin Muturi na Ekwe Ethuro
wa Bunge la Taifa na la seneti mtawalia wakiwa wa Jubilee. Kwa hivyo,
inatarajiwa kwamba ingawa Muungano wa Cord utakuwa upinzani kwa
Serikali, hautakuwa na uwezo wa kupinga masuala muhimu.
Kwa upande wake Rais Kenyatta na Naibu wake
William Ruto waliahidi kuhakikisha kwamba upinzani unakua wa maana
katika mabunge yote mawili na kwa Serikali kwa jumla.
“Walisema ni hamu yao kuona vyama vidogo vya upinzani vikitekeleza jukumu lao la kuiangalia Serikali ii isikiuke mipaka katika utendakazi wake,” alisema Onyango.
“Walisema ni hamu yao kuona vyama vidogo vya upinzani vikitekeleza jukumu lao la kuiangalia Serikali ii isikiuke mipaka katika utendakazi wake,” alisema Onyango.
Odinga alienda katika eneo Bunge la Khwisero
kaunti ya Kakamega, ambapo alimwambia Rais Kenyatta asinunue wabunge wa
Cord kuunga mkono upande wa Serikali.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: