Mfululizo wa mashambulizi nchini Iraq
Mashambulizi pia yalitokea katika mji wa Nassiriya
Umetokea mfululizo wa
mashambulio ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari , katika miji kadhaa
nchini Iraq asubuhi ya leo , wakati watu wakielekea kazini .
Mabomu hayo yamewauuwa takriban watu watano.
Watu wengi pia walijeruhiwa na idadi ya vifo
inatarajiwa kuongezeka. Mengi kati ya masambulio hayo yameripotiwa
katika mji mkuu Baghdad na mengine katika miji muhimu ukiwemo miji ya
Fallujah Kirkuk.
Mashambulio hayo yamekuja siku tano kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi wa majimbo ukiwa ni uchaguzi wa kwanza
kuendeshwa na taifa hilo tangu kuondoka kwa majeshi ya marekani mnamo
mwaka 2011 Kwa habari zaidi bofya hapa...>>>>>>>

Tanzanian Shilling Converter
No comments: