Mwanza: Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umeitaka polisi kufuata taratibu za kuhoji waandishi wa habar
Iwapo kuna jambo wanataka kujua ama hawaridhiki nalo
badala ya kukamata waandishi husika na kuwahoji kwa siri huku
likiwazuia kutoa taarifa za mahojiano yao.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan alisema
kawaida habari yoyote ambayo inakuwa imetumika katika chombo cha habari,
iwe na matatizo ama laa wanaopaswa kuisemea ni wahariri na siyo
waandishi wa habari.
Kwa hali hiyo ameitaka Polisi kuacha kuwahoji waandishi badala yake wawasiliane na wahariri wa vyombo husika.
“Tumestushwa sana na hatua hii ya Polisi, na
kutokana na kuwapo kwa taarifa za polisi kuwazuia wanaohojiwa kueleza
walichohojiwa jambo hili limezidi kuzua shaka na kutufanya kuamini
huenda hatua za kuwahoji waandishi wa habari Mtwara zina lengo la
maalumu kwa tasnia ya habari ama ni sehemu ya mkakati wa kufinya uhuru
wa habari,” alieleza.
Karsan alisema kitendo cha Polisi kumhoji
mwandishi namna hiyo ni makosa, na kusema iwapo walikuwa na jambo ambalo
walidhani haliko sawa kwa habari za waandishi hao walipaswa kupeleka
kwa wahariri au uongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari mikoani.
Polisi wanawahoji waandishi na watangazaji wa
redio kutokana na vurugu zilizotokea Januari 26 mwaka huu na kuendelea
kwa nyakati tofauti maeneo mbalimbali.
Mahakama na Halmashauri ya Wilaya ya
Masasi pamoja na magari 18 na pikipiki saba ziliteketezwa kwa moto na
wananchi ambao walidaiwa kupinga mradi usafirishaji wa gesi kutoka
Mtwara kwenda Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa toka Mtwara ilielezwa kuwa
waandishi ambao mpaka sasa wamehojiwa ni Andrew Mtuli wa Redio Pride FM,
ambaye anadai kuendesha kipindi cha Amka na Pride kinachorushwa na
redio hiyo kila siku alfajiri.
Wengine ni Emanuel Msigwa , Hasad Mdimu,
Philip Lulale na Mwandishi wa Magazeti ya Mwananchi Communications
Limited, Abdallah Bakari ambaye alitarajiwa kuhojiwa.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: