Tanzania haitishiki na kauli ya waasi ya kushambulia askari wa Tanzania
Serikali imesema haitasita kupeleka askari wake Jamhuri ya
Demokrasia ya Congo kwa ajili ya kukabiliana na waasi wa kikundi cha M23
.
Imesema hatua ya kikundi hicho kuionya Tanzania kutopeleka askari wake huko ni ya kutapatapa.
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene,
aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana asubuhi kuwa
Tanzania haitishiki na kauli ya waasi ya kushambulia askari wa Tanzania.
Alisema vitisho hivyo ni dalili za wazi kwamba waasi wanalijua Jeshi la Tanzania ndio maana wanatapatapa
Mwambene alisema Tanzania imeamua na itafanya kazi
hiyo kwa mwavuli wa Umoja wa Mataifa, lengo likiwa ni kuleta usalama
katika ebneo la Mashariki ya Congo.
Msemaji huyo alisema wanajeshi wa Tanzania wataungana na wanajeshi wa Afrika Kusini na Malawi katika operesheni hiyo muhimu.
Kauli hiyo inafuatia madai kuwa uongozi wa kikundi
hicho, umwandikia Rais Jakaya Kikwete, kumtaka afikirie upya wazo la
kuwapaleka askari wa Tanzania katika Brigedi ya Umoja wa Mataifa ya
kuwalinda raia katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
Tanzanian Shilling Converter
No comments: