Shirika la ujasusi la FBI nchini Marekani limesema linachunguza kile kinachodhania kuwa shambulio la kigaidi kufuatria mashambulizi mawili ya mabomu mwishoni mwa mbio za marathon za Boston
Ikiwa mashambulizi haya yatathibitishwa kuwa
mashambulizi ya kigaidi, basi yatakuwa mashambulizi mabaya zaidi
kushuhidiwa tangu yale ya Septemba 11 mwaka 2001
Mlipuko wa pili ulitokea sekunde chache tu baada
ya ule wa kwanza kutokea wakati mamia ya wanariadha wakikamilisha mbio
zao huku wakishangiliwa na umati. Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini
huku wengi wao wakitokwa na damu.
Rais Barack Obama amesisitiza kuwa serikali serikali itakahikisha kuwa washukiwa wa mashambulizi hayo lazima atakamatwa.
Picha na video kutoka Boston zilionyesha watu
wakiwa wamechanganyikiwa wasijue pa kwenda, huku magari ya huduma za
dharura yakielekea katika eneo la tukio na watu waliojeruhiwa vibaya
wakipelekwa kwenye hema la matibabu ya haraka.
"Kuna watu wengi wamelala chini," alisema mwanariadha mmoja akinukuliwa na chombo cha habari cha AP.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea saa tatu baada ya washindi kuvuka mstari wa ushindi.
"Kulikuwa na mlipuko, polisi, moto na EMS kwenye
eneo la tukio. Hatuna namna ya kufahamu namna watu walivyojeruhiwa,"
msemaji wa Polisi Boston alisema.
Shirika la habari la AP linasema kulikuwa na
sauti kubwa ya mlipuko upande wa kaskazini mwa mtaa wa Boylston Street,
karibu tu daraja linaashiria mstari wa kumalizia mashindano. Mlipuko
mwingine ukasikika dakika chache baadaye.
Mike Mitchell wa Vancouver kutoka Canada,
mwanariadha aliyemaliza kukimbia alisema alikuwa akiangalia nyuma ya
mstari wa kumalizia mashindano ndipo aliposikia ‘mlipuko mkubwa’
Inataarifiwa kuwa moshi ulipanda juu hewani
kiasi cha futi 50 (mita 15),' aliliambia shirika la habari la Reuters ,
na watu wakaanza kukimbia wakipiga mayowe baada ya kusikia
Tanzanian Shilling Converter
No comments: