TANGA:Wafanyabiashara na wakazi wa jijini Tanga, wameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupunguza bei za ving’amuzi
Kutokana na watu wengi kushindwa kumudu gharama zake.
TCRA, ilizima mitambo yake ya anolojia na kuwasha
ya digitali Februari Mosi mwaka huu kwa Mkoa wa Tanga na kuwafanya watu
wengi kukosa fursa ya kupokea matangazo na kupata habari.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wengi waliilalamikia TCRA kwa kuruhusu ving’amuzi kuuzwa kwa bei kubwa.
Waliishauri Mamlaka ya Mawasiliano kupunguza bei
ya ving’amuzi ili nao waweze kupokea matangazo katika televisheni zao
kwani kwa sasa zimebaki mapambo ndani ya majumba yao.
Bakari Mfaume ambaye ni mkazi wa Mwahako, alisema
Mamlaka ya Mawasiliano inapaswa kusimamia bei za ving’amuzi pamoja ili
bei yake iweze kuwa nafuu kwa watu wengi.
Akizungumzia kuhusu mazoea ya kupokea matangazo na
kupata habari kupitia televisheni zao, mkazi wa Sahare, Makame Kombo,
alisema sasa Watanzania wanarejeshwa kutoka zama za ukoloni ambako
walishasahau na hivyo kuitaka Serikali kuingilia kati.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: